سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
سورت 25

Al-Furqaan

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 41

وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا ٱلَّذِى بَعَثَ ٱللَّهُ رَسُولًا 41

{41} Yaani, "Na wanapokuona" ewe Muhammad, hawa wanaokukadhibisha, wanaokaidi ishara za Mwenyezi Mungu, watu wanaotakabari katika ardhi, wanakufanyia stihizai, na kukudharau, na wanasema kwa njia ya dharau na kukuona duni, "Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu alimtuma kuwa Mtume?" Yaani, haifai wala haiendani kamwe kwamba Mwenyezi Mungu amtume mwanamume huyu kama mtume! Na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa udhalimu wao na ukaidi wao, na kugeuzwa kwao uhakika wa mambo. Kwa maana, maneno yao haya yanaeleweka kwamba Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie ni duni zaidi na wa kudharauliwa mno, na kwamba kama ujumbe huu angekuwa amepewa mwingine, basi hilo lingefaa zaidi. "Na walisema: Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mwanamume mkubwa kutoka katika miji miwili hii?" Na maneno haya hayawezitoka isipokuwa kwa yule ambaye ni mjinga na watu wote na mpotevu zaidi yao, au yule ambaye ni mkaidi zaidi miongoni mwao. Naye ni mjinga, nia yake ni kuendeleza batili yake kwa kuikashifu haki na yule ambaye alikuja nayo. Vinginevyo, yeyote mwenye kutafakari hali za Muhammad bin Abdullah - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - atamkuta kwamba ndiye mwanamume bora wa walimwengu wote, na mtangulizi wao katika akili, elimu, ufahamu, maadili mazuri, na sifa nzuri mno, usafi, ujasiri, ukarimu, na maadili yote bora. Na kwamba mwenye kumdharau na kumdunisha, basi huyo amekusanya upumbavu, ujinga, upotovu, mkanganyiko, udhalimu, na kuvuka mipaka, ambayo hakuna mtu mwingine amewahi kuyakusanya. Basi na atosheke kwamba yeye ni mjinga na mpotofu katika kumtia dosari Mtume huyu mkuu, mbora, mtukufu, huku nia ya kutia dosari kwao huku ni kumfanyia stihizai, kuikakamia batili yao na kuwadanganya wale wenye udhaifu wa akili.