Al-Furqaan
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
يَوْمَ يَرَوْنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا 22
{22} "Siku watakapowaona Malaika" [ambao wao wenyewe waalipendekeza kwamba washuke], " hakutakuwa na furaha yoyote siku hiyo kwa wahalifu." Na hili ni kwa sababu hawatawaona kama wataendelea na uhalifu wao na ukaidi isipokuwa kwa ajili ya kuwaadhibu na kushukiwa na hali ngumu. Na ya kwanza ya hayo ni wakati wa kufa kwao wakati Malaika watakapowashukia. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na lau ungeliwaona madhalimu wakati wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake." Kisha katika kaburi ambapo watajiwa na Munkar na Nakir, wakawauliza juu ya Mola wao Mlezi, Nabii wao, na Dini yao, lakini hawatajibu jibu la kuwaokoa, kwa hivyo watafikwa na adhabu kali na kuondokewa na rehema. Kisha Siku ya Qiyama, ambapo Malaika watawaswaga kwenda Motoni, na kisha watakabidhiwa kwa walinzi wa Jahannamu, ambao watasimamia na kutekeleza adhabu juu yao. Basi haya waliyopendekeza, na haya waliyoomba, ikiwa wataendelea na uhalifu wao, basi hakuna budi watawaona na kukutana nao, na hapo watatafuta kujilinda kutokana na Malaika na kukimbia, lakini hawatakuwa na popote pa kukimbilia. "Watasema, Mwenyezi Mungu apishe mbali!" (Na kauli yake Mwenyezi Mungu) "Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kutoka nje ya mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya isipokuwa kwa kupewa mamlaka (na Mwenyezi Mungu)."