An-Noor
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
فِى بُيُوتٍ أَذِنَ ٱللَّهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا ٱسْمُهُۥ يُسَبِّحُ لَهُۥ فِيهَا بِٱلْغُدُوِّ وَٱلْـَٔاصَالِ 36
Kwa kuwa nuru ya imani na Qur-ani ni tukio la mara kwa mara la sababu zake katika misikiti, alizitaja, akizibainisha, na akasema:
{36} Yaani: Mwenyezi Mungu ndiye anayeabudiwa ''katika nyumba.'' Sehemu kubwa na kheri anazozipenda zaidi yeye, ni misikiti, ''Mwenyezi Mungu ameamrisha;'' yaani: ameamrisha na ameusia, ''zitukuzwe, na humo litajwe jina lake.'' Hizi ni jumla ya hukumu za misikiti, imejumuishwa katika kuiinua, kuijenga, kuifagia, kuisafisha kutokamana na najisi na udhia, na kuihifadhi na vichaa, na watoto wasiojilinda na najisi na kafiri, na ihfadhiwe na maneno ya upuuzi ndani yake na kunyanyua sauti bila kumtaja Mwenyezi Mungu. ''Na humo litajwe jina lake.'' Hii inajumuisha swala yote; Swala zake za faradhi na za Sunna, kusoma Qur-ani, kumtakasa Mwenyezi Mungu, kumsabihi Mwenyezi Mungu, na kusema Laa ilaaha illa Allah na aina nyinginezo za dhikri, na kujifundisha elimu na kuifundisha kwake, na kusoma ndani yake, na kukaa itkaaf, na ibada nyinginezo zinazofanywa misikitini. Na kwa hilo, kumekuwa kuimarisha Misikiti kumegawanyika sehemu mbili: kuimarisha majengo na kuyahifadhi, na kuimarisha kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu kutokamana na swala na mambo mengine, na hili ndilo tukufu zaidi kati ya aina hizi mbili. Na ndiyo maana zikaanzishwa na kuwekwa kama sheria swala tano na swala ya Ijumaa misikitini, ikalazimishwa kwa wengi katika wanavyuoni na ikapendekezwa kwa wanavyuoni wengine.