سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Taa-Haa
سورت 20

Taa-Haa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 71

قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ ۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَـٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِى جُذُوعِ ٱلنَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَآ أَشَدُّ عَذَابًا وَأَبْقَىٰ 71

{71} Kisha Firaun akawaambia wachawi: “Mlimwamini kabla sijawapa ruhusa?” Yaani, vipi mlimwaamini bila ya hakikisho wala ruhusa yangu? Jambo hili lilikuwa geni kwao kwa sababu ya uungwana wao kwake, unyonge wao, na kunyenyekea kwao katika kila jambo lao, na akalifanya hili kuwa miongoni mwa hayo. Kisha Firauni akarudi katika ukafiri wake na dhuluma yake baada ya dalili hii, na akayadharau waliyoyasema watu wake. Na akawaonyesha kuwa ushindi huu wa Musa dhidi ya wachawi haukuwa kwa sababu yeye ndiye mwenye haki, bali kwa sababu yeye na wachawi walikula njama na wakafanya njama ya kuwatoa Firauni na watu wake katika nchi yao. Basi watu wake wakaukubali upotovu huo kwake, na wakadhani ni kweli. "Basi akawadharau watu wake, wakamtii, hakika wao walikuwa ni watu walioukaa mipaka." Pamoja na maneno haya aliyoyasema, hayaingii akili mwa mtu yeyote ambaye ana akili kidogo na ujuzi wa ukweli. Kwani Musa alitoka Madyan peke yake, na alipofika; hakukutana na yeyote katika wachawi wala mwengine, bali aliharakisha kumwita Firauni na watu wake na akawaonyesha ishara. Firauni akayapa mgongo yale aliyokuja nayo Musa, basi akafanya alivyoweza, na akatuma mtu katika miji yake ili amkusanyie kila mchawi mjuzi, wakamjia. Na akawaahidi malipo na daraja juu ya ushindi, na walikuwa karibu kumshinda Musa; na yakatokea yale yaliyotea miongoni mwao. Basi je, inawezekana, au hata kufikirika kwamba wao na Musa walipanga na kukubaliana juu ya kile kilichotolewa? Hili ndilo lisilowezekana zaidi. Kisha Firauni akawatishia wachawi na akasema, nitawakateni "mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha." Kama afanyavyo shujaa kwa watu waovu; anakata mkono wake wa kulia na mguu wa kushoto. ''Na lazima nitawatundika misalabani katika vigogo ya mitende;'' ili muwe maarufu na mjulikane. "Kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake." Yaani, kwa madai yake na ya umma wake kwamba adhabu yake ni kali na ya kudumu kuliko ya Mungu. Ugeuzi wa ukweli, na vitisho kwa wale ambao hawana akili.