Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَآءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَـٰرِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ 84 ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَـٰرِهِمْ تَظَـٰهَرُونَ عَلَيْهِم بِٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَـٰرَىٰ تُفَـٰدُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ ٱلْكِتَـٰبِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْىٌ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلْعَذَابِ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ 85
(84-85) Na kitendo hiki kilichotajwa katika Aya hii ni kitendo cha wale waliokuwa katika wakati wa kuteremka kwa wahyi (ufunuo) huko Madina. Na hilo ni kwa sababu Aws na Khazraj - ambao ni Ansari - walikuwa washirikina kabla ya kitumilizwa kwa Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - na walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe kwa desturi ya Jahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu). Kwa hivyo, walishukiwa na makundi matatu ya Kiyahudi: Banu Quraydha, na Banu Nadhir, na Banu Qaynuqa'. Kwa hivyo, kila mojawapo ya makundi hayo likainigia katika mkataba na watu wa Madina. Basi wakawa wanapopigana vita, Mayahudi wanamsaidia yule waliyeingia naye katika mkataba dhidi ya wale wanaopigana nao, ambao wanasaidiwa na yale makundi mengine ya Mayahudi. Hivyo basi, Myahudi akawa anamuua Myahudi mwenzake, na anamtoa katika makazi yake kunapokuwa na kutolewa na uporaji. Kisha vita vinapopoa, na ikawa kulikuwa na mateka kati ya pande mbili, wanakomboana wenyewe kwa wenyewe. Na mambo hayo matatu yote walikuwa wamefaradhishiwa. Walifaradhishiwa kwamba wasimwage damu zao wenyewe kwa wenyewe, wala wasitoane wenyewe kwa wenyewe, na wakimkuta mateka miongoni mwao, lazima wamkomboe. Basi wakalifanyia kazi hilo la mwisho, na wakayaacha yale mawili ya kwanza. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakosoa katika hilo. "Je, mnaamini baadhi ya Kitabu" nalo ni kumfidia mateka "na mnakataa baadhi yake?" nalo ni kuua na kutoa nje. Na ndani yake kuna dalili ya kwamba imani inahitaji kufanya maamrisho na kuacha makatazo. Na kwamba maamrisho ni katika imani. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Basi ni nini malipo ya mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila aibu katika maisha ya duniani" Na hilo lilikwishafanyika, na Mwenyezi Mungu akawafedhehesha, na akampa nguvu Mtume wake dhidi yao, hivyo, (Mtume) akawauwa aliouwaua. Na akawateka aliowateka miongoni mwao, na akawafukuzilia mbali wale aliofukuzilia mbali. "Na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda." Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza sababu iliyowalazimu kukufuru baadhi ya Kitabu na kuamini baadhi yake, akasema: