سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورت 2

Al-Baqara

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 41

وَءَامِنُوا۟ بِمَآ أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوٓا۟ أَوَّلَ كَافِرٍۭ بِهِۦ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِى ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّـٰىَ فَٱتَّقُونِ 41

(41) “Na aminini niliyoyateremsha,” nayo ni Qur-ani ambayo aliiteremsha kwa mja wake na Mtume wake Muhammad rehema ana amani ziwe juu yake. Basi akawaamrisha kuiamini, na kuifuata. Na hilo linalazimisha kumwamini yule aliyeteremshiwa juu yake. Na akataja sababu ya kuwafanya waamini. Akasema: “ambayo yanasadikisha mliyo nayo.” Yani yanayokubaliana nayo, na hayatofautiani nayo; hivyo basi hamna kizuizi cha kutomuamini, kwa sababu kilikuja na waliyokuja nayo Mitume. Basi nyinyi ndio mnastahiki zaidi kukiamini na kukisadiki, kwa sababu nyinyi ni watu wa vitabu na elimu. Pia katika kauli yake: “ambayo yanasadikisha mliyo nayo,” kuna ishara kwamba msipokiamini, hilo litawarudia wenyewe kwa kumaanisha mnayakanusha yale mliyo nayo. Kwa maana yale ambayo kilikuja nayo ndiyo Musa alikuja nayo, na Isa na wengineo miongoni mwa Manabii. Hivyo basi, kukikanusha kwenu ni kukataa yale mliyo nayo. Pia, katika vitabu vilivyo mikononi mwenu kuna sifa za Nabii huyu ambaye alikuja na Qur-ani hii, na bishara yake. Kwa hivyo, msipoiamini, mtakuwa mmekadhibisha baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yenu. Na mwenye kukadhibisha baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yake, basi kwa hakika atakuwa amekadhibisha yote. Kama vile mwenye kumkufuru Mtume mmoja, basi kwa hakika atakuwa amewakufuru Mitume wote. Alipowaamrisha kumwamini, akawakataza na akawaonya kinyume chake, nacho ni kuikufuru. Akasema: “Wala msiwe wa kwanza kuyakufuru.” Yani Mtume na Qur-ani. Na katika kauli yake: “Wa kwanza kuyakufuru” ina ufasaha zaidi kuliko kauli yake, “wala msikikufuru” kwa sababu, ikiwa watakuwa wa kwanza kukikufuru, basi itakuwa katika hili kukimbilia kwao kukikufuru, kinyume cha kinachowapasa, na dhambi zao zikawa juu yao na dhambi za mwenye kuwafuata baada yao. Kisha akataja kinachowazuia kuamini, ambacho ni kuchagua anasa ya chini kuliko furaha ya milele. Akasema, "Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo." Ambayo ni kile wanachopata miongoni mwa vyeo na vyakula ambavyo wanadhani kuwa vitakatika ikiwa watamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi wakavinunua kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakavipenda na kuvipendelea. "Na Mimi tu." Yani siyo mwingine, "nicheni;" kwa sababu ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu peke yake, basi huko kumcha kutawalazimu kutanguliza mbele kuziamini Ishara zake badala ya thamani ndogo. Kama vile ikiwa mtachagua thamani hiyo ndogo; basi hiyo ni dalili ya kuondoka kwa uchamungu kutoka katika nyoyo zenu. Kisha akasema: