سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورت 2

Al-Baqara

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 256

لَآ إِكْرَاهَ فِى ٱلدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشْدُ مِنَ ٱلْغَىِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِٱلطَّـٰغُوتِ وَيُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسْتَمْسَكَ بِٱلْعُرْوَةِ ٱلْوُثْقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَا ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 256

{256} Huku ni kubainisha ukamilifu wa dini hii ya Uislamu, na kwamba ni sababu ya ukamilifu wa dalili zake, na uwazi wa Aya zake. Na kwa kuwa ni Dini ya akili na elimu, na Dini ya fitra (umbile la asili), na hekima, Dini ya wema na urekebishaji, na Dini ya haki na uongofu. Na kwa ukamilifu wake na kukubaliwa na fitra (umbile la asili), haihitaji kulazimisha juu yake. Kwa sababu, kulazimisha kunakuwa tu kwa kile ambacho nyoyo zimejitenga nacho, na kinapingana na uhakika na haki. Au kile ambacho dalili zake na aya (ishara) zake zimefichika, na vinginevyo. Mwenye kujiwa na dini hii naye akaikataa na wala asiikubali, basi hilo ni kwa sababu ya ukaidi wake. Kwani, “uwongofu umekwisha pambanuka kutokana na upotovu;” na mtu yeyote hajabaki na kisingizio wala hoja yoyote ikiwa ataikataa na asiikubali. Na wala hakuna upinzani baina ya maana hii na Aya nyingi zinazolazimu kuwepo kwa Jihadi. Kwani, Mwenyezi Mungu ameamrisha kupigana vita ili Dini yote iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kuzuia uadui wa wenye kufanya uadui dhidi ya dini. Waislamu wamekubaliana kwamba jihadi itaendelea kuwepo pamoja na (kiongozi) mwema na muovu. Na kwamba miongoni mwa faradhi zinazoendelea ni Jihadi ya kimaneno na Jihadi ya kimatendo. Na mwenye kudhani kwamba Aya hii inapingana na Aya za Jihadi, kwa hivyo akawa na uhakika kuwa ilifutwa; basi kauli yake hiyo ni dhaifu kimaandiko na kimaana. Kama ilivyo dhahiri na bainifu kwa mwenye kuitafakari Aya hii tukufu, kama tulivyoashiria hilo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kugawanyika kwa watu katika makundi mawili: Kundi lililomwamini Mwenyezi Mungu peke yake bila ya mshirika yeyote na likakufuru Taaghut. – Nayo ni kila lenye kupingana na imani juu ya Mwenyezi Mungu kama vile shirki na mengineyo. Basi huyo bila ya shaka, “amekamata kishikio madhubuti” ambacho hakiwezi kuvunjika. Bali yeye amenyooka kwenye Dini sahihi mpaka afike kwayo kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake. Na kundi la pili linachukuliwa kutoka katika maana isiyo ya moja kwa moja ya aya. Kwamba asiyemwamini Mwenyezi Mungu, bali alimkufuru na akamuamini Taaghut; basi yeye ataangamia milele na ataadhibiwa adhabu ya milele. Na kauli yake, “na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema” yani sauti zote katika lugha mbalimbali, kwa mahitaji mbalimbali. Na ni mwenye kusikia dua ya waombaji dua, na kunyenyekea kwa wanaonyenyekea. “Mwenye kujua vyema” yale yaliyofichwa na vifua, na yale yanayofichika katika mambo ya siri. Kisha anamlipa kila mtu kulingana na anayojua katika nia zake na matendo yake.