سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورت 2

Al-Baqara

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 183

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ 183

({83} Mola Mtukufu anatoa habari yale aliyowaneemesha kwayo waja wake kwamba aliwafaradhishia kufunga Saumu kama alivyoifaradhisha kwa umma zilizopita. Kwa sababu ni miongoni mwa sheria na maamrisho ambayo ni masilahi ya viumbe katika nyakati zote. Na ndani yake kuna kuuhimiza umma huu kwamba mnapaswa mshindane na wengineo katika kukamilisha matendo, na kuharakisha kuziendea sifa zilizo njema; na kwamba siyo katika mambo mazito ambayo ni mahususi kwenu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hekima yake katika kuweka sheria ya kufunga Saumu akasema, “ili mpate kumcha Mungu.” Kwa sababu kufunga saumu ni miongoni mwa sababu kubwa za uchamungu. Kwa sababu ndani yake kuna kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake. Na katika yale inayojumuisha ya uchamungu ni kuwa mtu mwenye Saumu anaacha yale ambayo Mwenyezi Mungu amemharamishia katika kula, kunywa, kujamiiana na mfano wake, ambayo nafsi yake huyaelekea. Akifanya hivyo ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu, akitaraji malipo yake kwa kuyaacha, na hilo ni katika uchamungu. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye Saumu anaizoesha nafsi yake juu ya kumchunga Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi anaacha kile kinachotamaniwa na nafsi yake ijapokuwa ana uwezo juu yake, kwa sababu anajua kwamba Mwenyezi Mungu anamwona. Na miongoni mwake ni kwamba Saumu hupunguza njia za Shetani. Kwa maana, yeye (Shetani) hupita katika mwanadamu kama kupita kwa damu, kwa hivyo kwa kufunga Saumu, athari zake hudhoofika, na dhambi zinapungua kutoka kwake. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kufunga Saumu mara nyingi utiifu wake huwa mwingi. Na mambo ya utiifu ni miongoni mwa sifa za uchamungu. Na miongoni mwake ni kwamba, tajiri anapoonja uchungu wa njaa, hilo linamlazimu kuwafariji mafukara wasiokuwa na kitu. Na hilo ni katika sifa za uchamungu.