Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
لَّيْسَ ٱلْبِرَّ أَن تُوَلُّوا۟ وُجُوهَكُمْ قِبَلَ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ ٱلْبِرَّ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلْكِتَـٰبِ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ وَءَاتَى ٱلْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ ذَوِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينَ وَٱبْنَ ٱلسَّبِيلِ وَٱلسَّآئِلِينَ وَفِى ٱلرِّقَابِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَـٰهَدُوا۟ ۖ وَٱلصَّـٰبِرِينَ فِى ٱلْبَأْسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَحِينَ ٱلْبَأْسِ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُوا۟ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُتَّقُونَ 177
(177) Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema: “Siyo wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi.” Yani huu siyo wema uliokusudiwa kutoka kwa waja. Ndiyo inakuwa kufanya utafiti mwingi na mjadala juu yake ni katika kusumbukana ambako, hakuna kitu chini yake isipokuwa upinzani na hitilafu tu. Na hili ni sawa na kauli yake, (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. “Mwenye nguvu siyo mwenye kuwapiga watu miereka. Lakini mwenye nguvu ni yule anayejidhibiti nafsi yake anapokasirika,” na mfano wake. “Bali wema ni wa anayemuamini Mwenyezi Mungu” yani kwamba yeye ndiye Mungu mmoja. Anayesifika kwa kila sifa ya ukamilifu, aliyetakasika na kila upungufu. “Na Siku ya Mwisho” nayo ni kila aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. Au aliyoyaeleza Mtume wake kuhusu yatakayotokea baada ya kufa. “Na Malaika” ambao Mwenyezi Mungu aliotueleza katika Kitabu chake na aliowaeleza Mtume wake rehema na amani zimshukie. “Na Kitabu,” yani vitabu vyote ambavyo Mwenyezi Mungu alivyoteremsha kwa Mtume wake. Na kitukufu zaidi kati yake ni Qur-ani. Basi ayaamini yaliyomo katika habari zake na hukumu zake, “na Manabii” kwa ujumla. Hususan wa mwisho wao na mbora wao wote, Muhammad rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. “Na akawapa mali.” Nayo ni kila anachokichuma mtu katika mali, sawa iwe kidogo au nyingi. Yani akatoa mali “licha ya kuipenda kwake,” yani kuipenda mali. Hivyo akabainisha hapa kwamba mali inapendwa na nafsi, na hakaribii mja kuitoa. Kwa hivyo, mwenye kuitoa licha ya kuipenda ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi huu ni uthibitisho wa imani yake. Na katika kutoa mali licha ya kuipenda ni kwamba atoe sadaka hali ya kuwa ni mwenye afya nzuri, bahili mwenye utu nayo; hali ya kuwa anatarajia utajiri, anachelea umasikini. Kadhalika, ikiwa atatoa sadaka katika hali ya upungufu, inakuwa bora zaidi, kwa sababu katika hii hali, anapenda kuizuilia, kwa kile anachofikiri kuhusiana na kuikosa na ufukara. Na vivyo hivyo katika kutoa chenye thamani katika mali, na anachokipenda katika mali yake, kama alivyosema Aliyetukua. “Kamwe hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda.” Na hawa wote ni katika wale waliotoa mali pamoja na kuipenda. Kisha akataja wanaopewa. Nao ni wale watu wanaostahiki zaidi wema wako na ihsani yako, miongoni mwa jamaa ambao inakuumiza misiba yao, na unafurahia kwa furaha yao. Ambao wanasaidiana na wanasaidiana kutoa fidia ya mauaji. Basi katika wema ulio bora zaidi na kamilifu ni kuwahudumia jamaa kwa ihsani ya kimali na kikauli, kulingana na ukaribu wao na haja yao. Na pia mayatima ambao hawana mwenye kuwachumia. Na wala hawana uwezo wa kujitosheleza kwao. Na hii ni kutokana na rehema yake [Mwenyezi Mungu Mtukufu] kwa waja wake, ambayo inaonyesha kuwa Yeye ni mwenye rehema (huruma) zaidi kwao kuliko baba kwa mtoto wake. Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake, na akawafaradhishia katika mali zao kuwafanyia wema waliofiwa na wazazi wao, ili wawe kama wale ambao hawakupoteza wazazi wao. Na kwa sababu malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa hivyo, mwenye kumrehemu yatima wa asiyekuwa yeye, yatima wake atarehemewa. “Na masikini,” nao ndio wale ambao haja imewatuliza, na ufukara ukawadhalilisha. Basi wanayo haki juu ya matajiri kwa kile chenye kuondosha umasikini wao au kuupunguza. Kwa kile wanachoweza, na kwa kile kilicho chepesi. “Na wasafiri,” naye ni mgeni aliyekatikiwa katika nchi isiyokuwa ya nchi yake. Basi Mwenyezi Mungu akawahimiza waja wake wampe katika mali kile chenye kumsaidia katika safari yake, kwa sababu yeye kwa kawaida huwa na mahitaji, na mwenye gharama nyingi. Kwa hivyo, ni juu ya yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa neema ya kuwa katika nchi yake na raha yake. Na akampa katika neema zake amrehemu ndugu yake mgeni, ambaye yuko katika sifa hizi kulingana na uwezo wake. Hata kama ni kwa kumpatia chakula cha njiani au kumpa chombo kwa ajili ya safari yake, au kumzuilia kinachompa katika dhuluma na mengineyo. “Na waombao,” yani wale wanaopatwa na haja miongoni mwa haja ambazo zinawalazimu kuomba. Kama vile yule aliyepewa mtihani wa kulipa fidia ya kufanya kosa la jinai au kodi anayolazimika kuwalipa viongozi. Au anayewaomba watu ili kuimarisha masilahi ya umma kama vile misikiti, shule, madaraja na mfano wake. Basi huyu ana haki (ya kupewa) hata kama ni tajiri. “Na katika ukombozi,” basi anaingia humo kumweka huru mtumwa na kumsaidia. Na kumpa mali Al-mukaatab (yule aliyeandikiana na bwana wake kujilipia pole pole mali ya kujikomboa) ili amtimizie bwana wake. Na kuwakomboa mateka wa vita kutoka kwa makafiri au kutoka kwa madhalimu. “Na akashika Swala na akatoa Zaka.” Na haya yalikwisha tangulia mara nyingi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweka pamoja swala na zaka. Kwa sababu hizo ndizo ibada bora zaidi. Na mambo ya kujiweka karibu kwa Mwenyezi Mungu kwayo yaliyo kamili zaidi ni ibada za moyoni, kimwili, na kimali. Na kwazo inapimwa imani, na inajulikana kwazo yakini ya mwenye hivyo. “Na wanaotimiza ahadi yao wanapoahidi.” Na ahadi ni kutekeleza alichowajibisha Mwenyezi Mungu au alichojiwajibishia mja mwenyewe. Basi akaingia katika hilo haki zote za Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewawajibishia hizo waja wake. Nao wakaziitikia basi wanalazimika kuzitimiza, na wakaingia chini ya ahadi yake, na ikawa ni wajibu kwao kuzitekeleza. Na haki za waja ambazo Mwenyezi Mungu aliziwajibisha juu yao. Na haki ambazo mja alijilazimishia mwenyewe kama vile viapo na nadhiri, na mfano wake. “Na wanaovumilia katika shida.” Yani ufukara, kwa sababu fukara anahitaji subira katika njia nyingi. Kwa sababu anapatwa na maumivu yenye kuendelea ya kimoyo na kimwili ambayo hayamfikii asiyekuwa yeye. Kwa maana, matajiri wakifurahia kwa kile asichoweza kukipata, anaumia. Na akipata njaa au watoto wake wakipatwa na njaa, anaumia. Na akila chakula kisichoendana na matamanio yake, anaumia. Na akiwa uchi au akakaribia kuwa uchi, anaumia. Na akitazama kilichoko mbele yake (cha sasa) na kile anachofikiria kukipata wakati ujao anaojitayarisha kwa ajili yake, anaumia. Na akipatwa na baridi ambayo hawezi kuizuia, anaumia. Basi haya yote na mfano wake ni taabu anazoamrishwa kuwa na subira juu yake. Kutumaini na kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yake. “Na dhara,” yani maradhi kwa aina zake tofauti tofauti. Kuanzia homa, vidonda, upepo, na maumivu ya viungo, hata jino na kidole, na mfano wake. Yeye kwa hakika anahitaji subira kwa hayo. Kwa sababu, nafsi inadhoofika, na mwili unauma, na hilo ni gumu mno kwa nafsi, hasa ikiwa ni kwa muda mrefu. Hivyo basi ameamrishwa kuwa na subira, kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. “Na wakati wa vita,” yani wakati wa kupigana na maadui walioamrishwa kupigana nao. Kwa sababu, kusimama imara ni kugumu sana juu ya nafsi. Na mtu anahuzunika kwa sababu ya kuuawa, au kujeruhiwa, au kushikwa mateka. Kwa hivyo, anahitaji subira katika hayo akitarajia na kutumaini malipo ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. Ambaye ushindi na usaidizi ni kutoka kwake, ambao aliwaahidi wenye subira. “Hao,” yani wale wanaosifika kwa yale yaliyotajwa ya imani njema, na matendo ambayo ni athari ya imani, na uthibitisho wake, na nuru yake. Na maadili ambayo ni uzuri wa mwanadamu na uhakika wa ubinadamu, basi hao “ndio waliosadikisha” katika imani yao. Kwa sababu matendo yao yalisadikisha imani yao, “na hao ndio wachamungu” kwa sababu waliacha makatazo, na wakafanya maamrisho. Kwa sababu mambo haya yanajumuisha sifa zote za heri kwa ndani yake na kwa kile zinazolazimu. Kwa sababu kutimiza ahadi kunajumuisha dini nzima, na kwa sababu ibada zilizotajwa katika Aya hii ndizo ibada kubwa kabisa. Na atakayezifanya, atasimama bora zaidi kwa zinginezo. Basi hao ndio watu wema, wakweli, wachamungu. Na imekwisha julikana kile alichoyawekea Mwenyezi Mungu mambo haya matatu ya malipo ya kidunia na ya kiakhera. Ambayo haiwezekani kuyabainisha kwa kina katika [mfano wa] mahali hapa.