Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
إِنَّ فِى خَلْقِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱخْتِلَـٰفِ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱلْفُلْكِ ٱلَّتِى تَجْرِى فِى ٱلْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن مَّآءٍ فَأَحْيَا بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٍ وَتَصْرِيفِ ٱلرِّيَـٰحِ وَٱلسَّحَابِ ٱلْمُسَخَّرِ بَيْنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ 164
(164) Mwenyezi Mungu Mtukufu anatoa habari kwamba katika hivi viumbe vikubwa kuna ishara; yani dalili za upweke wa Muumba mwanzilishi, Uungu wake, Ukubwa wa mamlaka yake, Rehema zake, na Sifa zake zinginezo. Lakini ni, “kwa watu wanaozingatia” yani kwa wale wenye akili wanaozitumia katika yale zilizoumbiwa kwa ajili yake. Basi kwa kadiri Mwenyezi Mungu alivyompa mja wake katika akili, ananufaika kwa hizi Aya na anazijua kwa akili yake, na fikira yake na kuzingatia kwake. Na katika, “hakika, katika kuumbwa kwa mbingu” katika kuinuka kwake, upana wake, kuimarika kwake, na kutengenezeka kwake vizuri. Na kile Mwenyezi Mungu alichoweka ndani yake kama jua, na mwezi, na nyota, na mpangilio wake wa masilahi ya waja. Na katika uumbaji wa, “ardhi” kama tandiko kwa viumbe, wanaweza kutulia juu yake na kunufaika na vile vilivyo juu yake na kuzingatia. Hayo yanaonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji, uendeshaji wa mambo, na kubainisha uwezo wake mkubwa ambao kwao aliiumba. Na hekima yake ambayo kwayo aliitengeneza sawasawa, na akaifanya kuwa vizuri, na akaipanga. Na elimu yake na rehema zake ambazo kwazo aliweka ndani yake kile alichoweka miongoni mwa manufaa ya viumbe, masilahi yao, mahitaji yao ya lazima na mahitaji yao ya kawaida. Na katika hilo, kuna dalili kubwa mno ya ukamilifu wake na kustahiki kwake kupwekeshwa katika ibada kwa sababu ya upweke wake katika kuumba, kuendesha na kusimamia mambo ya waja wake. Na katika, “kukhitalifiana usiku na mchana.” Nako ni kufuatana kwake kwa kuendelea, moja yake inapoondoka, nyingine huifuata. Na katika kutofautiana kwake katika joto, baridi, wastani, urefu, ufupi, na kuwa kati na kati na majira yanayotokea kutokana na hayo. Ambayo kwayo masilahi ya wanadamu na wanyama wao yanapangika vizuri. Na kila kilichoko juu ya uso wa ardhi, kama vile miti na mimea, vyote hivyo ni kwa mpangilio, uendeshaji, na kuvifanya kutii, hayo yote akili zinashangazwa kwayo. Na haziwezi kueleweka na wanaume wenye nguvu, ambayo yanaonyesha uwezo wa mwendeshaji wake, na elimu yake, na hekima yake, na rehema yake pana. Na upole wake wenye kujumuisha, na utendaji wake na utendeshaji wake ambao yu pekee katika hilo. Na ukuu wake, na ukuu wa ufalme wake na mamlaka yake, ambayo inamlazimu kwamba afanyiwe yeye uungu na aabudiwe. Na apwekeshwe katika upendo na utukufu, na khofu na matumaini, na kufanya juhudi katika anayopenda na kuridhia. Na katika, “marikebu ambazo hupita baharini.” Nazo ni safina na majahazi na mfano wake, ambayo Mwenyezi Mungu aliwafunulia waja wake namna ya kuyatengeneza. Na akawaumbia ala za ndani na nje zilizowawezesha kufanya hivyo. Kisha akaitiisha bahari hii kuu na pepo ambavyo vinazibeba (marikebu) pamoja na vilivyomo kama vile abiria, mali, na bidhaa ambazo ni miongoni mwa manufaa ya watu; na zinazowahudumia masilahi yao na yanapangika maisha yao. Basi ni nani aliyewafunulia namna ya kuzitengeneza, na akawawezesha kufanya hivyo, na akawaumbia ala ambazo kwazo wanaweza kuziunda? Au ni nani aliyeitiisha bahari kwa ajili yake, zinapita humo kwa idhini yake, na kutiisha kwake, na pepo? Au ni nani aliyeumbia vyombo vya nchi kavu na vya baharini moto na madini vinavyosaidia kuvibeba (vyombo) na kubeba mali zilizomo ndani yake? Basi je, mambo haya yalitokea tu kwa sadfa, au vilitengenezwa na huyu kiumbe dhaifu peke yake asiyekuwa na uwezo. Ambaye alitoka katika tumbo la mama yake bila ya kuwa na elimu wala uwezo, kisha Mola wake Mlezi akamuumbia uwezo. Na akamfundisha alichotaka kumfunza, au aliyevitiisha hivi ni Mola Mlezi Mmoja, Mwenye hekima na elimu, asiyeshindwa na chochote, na wala hakizuiki chochote kwake? Bali mambo yote yako chini ya uungu wake, na yameutii ukuu wake, na yameunyenyekea uwezo wake. Na mwisho wa mja huyu dhaifu ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfanya kuwa sehemu katika sehemu za sababu ambazo kwazo mambo haya makubwa yanapatikana. Na hili linaashiria rehema ya Mwenyezi Mungu na kuwatunza kwake viumbe wake. Na hilo linalazimu kwamba mapenzi yote yawe kwake, na hofu, na matumaini, na utiifu wote, unyenyekevu na utukufu. "Na maji anayoteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni," nayo ni mvua ishukayo kutoka katika mawingu. "Na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake." Kwa hivyo ikadhirisha aina za vyakula na sampuli za mimea ambavyo ni katika mahitaji ya lazima ya viumbe ambavyo hawawezi kuishi bila hivyo. Je, huo sio ushahidi wa uwezo wa yule aliyeyateremsha na akatoa kwayo alichokitoa? Na rehema zake na upole wake kwa waja wake, na kuwatimizia maslahi yao, na ukubwa wa kumhitaji kwao, na udharura wao kwake kwa njia zote? Je, hilo halihitaji kwamba awe mwabudiwa wao na Mungu wao? Je, huo sio ushahidi wa kuwafufua wafu na kuwalipa kwa matendo yao? “Na akaeneza humo,” yani katika ardhi “katika kila aina ya wanyama.” Yani alieneza katika maeneo ya ardhi wanyama mbalimbali ambayo ni dalili juu ya uwezo wake, utukufu wake, upweke wake, na mamlaka yake makubwa. Na aliwatiisha (viumbe hao) kwa watu ili wanufaike kwayo kwa njia zote za kunufaika. Miongoni mwake kuna wale wanaokula katika nyama yake, na wanakunywa katika maziwa yake. Na miongoni mwake kuna wale wanaowapanda. Na miongoni mwake kuna wale wanaotumika katika masilahi yao na ulinzi wao. Na miongoni mwake kuna wale ambao ni mazingatio. Na miongoni mwake ni kuwa ameeneza humo katika kila mnyama, kwani Yeye, aliyetakasika ndiye anayesimamia riziki zao, na anajua makao yake na mapitio yake. “Na katika mabadiliko ya pepo” (ambazo huwa) baridi na moto, kusini na kaskazini, mashariki na magharibi, na kati ya hayo. Na wakati mwingine huyatimua mawingu, na wakati mwingine huambatanisha kati yake. Na wakati mwingine huichavusha, na wakati mwingine husababisha mvua, na wakati mwingine huipasua na huondoa madhara yake. Na wakati mwingine huwa ni rehema, na wakati mwingine hutumwa ili kuadhibu. Basi ni nani aliyezibadilisha huku kubadilika. Na akaweka ndani yake katika manufaa ya waja ambayo hawawezi kufanya bila hayo? Na akazitiisha ili wanyama wote waishi humo, na ili miili, miti, nafaka na mimea viwe bora isipokuwa kwa Mwenye nguvu, Mwenye hekima, Mwingi wa huruma, Mpole kwa waja wake. Ambaye anastahiki kudhalilikiwa kwote, kunyenyekewa, upendo, kurudi kwake (toba), na kuabudiwa? Na katika kuyatiisha mawingu baina ya mbingu na ardhi, licha ya wepesi na wembamba wake, hubeba maji mengi. Basi Mwenyezi Mungu huyapeleka popote apendapo, na kuihuisha nchi na watu kwayo. Na anamwagilia milima na mabonde, na kuiteremsha kwa watu wakati wanayahitaji. Basi ikiwa wingi wake unawadhuru, yeye huishikilia isiwanyee, kisha huiteremsha kwa rehema na upole, na huiondoa kwa kuwajali na kuwahurumia. Basi ni ukubwa ulioje wa Mamlaka yake, na wema (ukarimu) mwingi ulioje, na upole zaidi wa neema. Je, siyo jambo baya mno kwa waja wake kufurahia riziki yake na kuishi kwa wema wake, huku wakijiasaidia na hayo katika kumkasirisha na kumuasi? Je, hiyo siyo dalili ya stahamala yake na subira yake? Na msamaha wake na kuachilia kwake mbali (makosa) na ukubwa wa upole wake? Basi ni zake sifa njema mwanzo na mwisho, ndani na dhahiri. Na jumla ya hayo ni kwamba kila mtu mwenye akili timamu anavyotafakari katika hawa viumbe. Na mawazo yake yakapenya ndani ya maajabu ya uumbaji. Na kila anavyozidi kutafakari katika ufundi na kile alichowekwa ndani yake katika wema na hekima zinazopendeza, atajua kwa hayo kwamba, viliumbwa kwa ajili ya haki na kwa haki. Na kwamba ni karatasi za Aya (ishara) na vitabu vya dalili za yale aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu juu ya nafsi yake na upweke wake. Na yale waliyosimulia Mitume kuhusu Siku ya Mwisho. Na kwamba vimetiishwa na wala havina utendaji wala ugumu wowote kwa mpangaji wake na mwendeshaji wake. Basi utajua kwamba ulimwengu wa juu na wa chini wote ni wenye kumuhitajia Yeye, na kwake wanakusudia. Na kwamba Yeye ndiye Aliyejitosheleza kwa dhati yake kutokana na viumbe vyote, hapana mungu ila Mwenyezi Mungu. Basi hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hapana mola mlezi isipokuwa Yeye.