Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
إِنَّآ أَرْسَلْنَـٰكَ بِٱلْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْـَٔلُ عَنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْجَحِيمِ 119
Kisha Mtukufu akataja baadhi ya Aya zilizofupishwa, zenye kujumuisha aya ambazo zinaonyesha ukweli wake - rehema na amani ziwe juu yake - na usahihi wa kile alichokuja nacho, akasema:
(119) "Hakika Sisi tumekutuma kwa haki uwe mbashiri, na mwonyaji." Na hii (Aya) imejumuisha ishara alizokuja nazo. Nazo zinarudi kwa mambo matatu: La kwanza ni kumtuma kwenyewe. Nalo la pili ni katika siira (maisha) yake, muongozo wake, na welekezi wake. Na la tatu ni katika kujua yale aliyoleta katika Qur-ani na Sunnah. Hivyo, la kwanza na la pili yanaingia katika kauli yake: "Hakika Sisi tumekutuma". Nalo la tatu [linaingia] katika kauli yake: "Kwa haki". Na kubainisha jambo hilo la kwanza - ambalo ni kutumwa kwake kwenyewe - ni kwamba Yeye alishajua hali ya watu wa ardhini kabla ya kumtuma kwake - rehema na amani ziwe juu yake.- Na yale waliyokuwa juu yake ya kuabudu masanamu, moto na misalaba, na kubadilisha dini zao mpaka wakawa katika giza la ukafiri lililowajumuisha na kuwaenea, isipokuwa mabaki ya Watu wa Kitabu waliokuwa wametoweka kabla ya utume wake. Na ilikwisha julikana kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaumba viumbe wake bure, na wala hakutelekeza. Kwa sababu, Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye elimu, Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu. Kwa hivyo, katika hekima yake na rehema zake kwa waja wake, ni kuwa aliwatumia huyu Mtume mtukufu akiwaamrisha kumwabudu Mwingi wa Rehema peke yake, asiyekuwa na mshirika. Basi kwa kumtuma tu, mwenye akili timamu anaujua ukweli wake, nao ni dalili kubwa ya kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ama la pili, mwenye kumjua Nabii – rehema na amani ziwe juu yake – kumjua kukamilifu, na akajua siira (maisha) yake na mwenendo wake kabla ya utume na kuinukia kwake juu ya sifa kamilifu zaidi. Kisha baada ya hapo heshima yake kubwa na maadili yake yanayoshangaza watazamaji yakaongezeka. Kwa hivyo, mwenye kujua hayo na kukusanya vyema hali zake, atajua kwamba sio chochote ila ni maadili ya Manabii wakamilifu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alizifanya sifa za mtu (kitu) kuwa ushahidi mkubwa zaidi ya kuwajua wenyewe, na ukweli wao na uongo wao. Na ama la tatu ni kujua aliyoyaleta - rehema na amani ziwe juu yake.- Yale ya sheria kuu na Qur-ani Tukufu, inayojumuisha habari za kweli, maamrisho mazuri, kukataza maovu yote, na miujiza ya kuvutia. Hivyo basi, ishara zote zinaingia katika haya matatu. Kauli yake "uwe mbashiri," yani kwa mwenye kukutii kuwa atapata furaha ya duniani na ya Akhera. "Mwonyaji" kwa mwenye kukuasi kuwa atapata taabu na maangamivu ya duniani na ya Akhera. "Na wala hutaulizwa juu ya wenzi wa Moto." Yani wewe hutaulizwa juu yao. Juu yako wewe ni kufikisha (ujumbe), na juu yetu ni hisabu.