Al-Kahf
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِى هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَكْثَرَ شَىْءٍ جَدَلًا 54
{54} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wa Qur-ani, na utukufu wake, na ujumla wake, na kwamba ameeleza ndani yake "kila namna ya mfano." Yaani, kila njia zenye kufikisha kwenye elimu zenye manufaa na furaha ya milele na kila njia inayokinga kutokana na uovu na maangamivu. Basi ndani yake kuna mifano ya halali na haramu, malipo ya matendo, kutia moyo na kutishia, na habari za ukweli zenye kunufaisha nyoyo kiitikadi na utulivu na nuru. Na haya ni katika yale yanayolazimu kujisalimu kwa Qur-ani hii na kuipokea kwa kuifuata na kuitii na kutobishana nayo katika jambo lolote lile. Lakini pamoja na hayo, wengi wamekuwa wakibishana juu ya haki baada ya kudhihirika kwake, na hubishana kwa batili ili waivunje haki kwayo. Na ndio maana akasema, “Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi." Yaani, kujadili na kubishana juu yake, pamoja na hayo hayawafailii, wala sio waadilifu katika hayo. Na kilichomsababishia hayo na kutomuamini Mwenyezi Mungu, ni dhuluma tu na ukaidi, si kwa sababu ya kuwepo upungufu wowote katika kubainisha kwake, na hoja zake, na uthibitisho wake. Vinginevyo, lau kuwa ingewajia adhabu na yakawafikia yale yaliyowafikia wa kabla yao, basi hii isingekuwa hali yao. Na ndiyo maana akasema: