Yunus
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِى وَتَذْكِيرِى بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوٓا۟ أَمْرَكُمْ وَشُرَكَآءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ ٱقْضُوٓا۟ إِلَىَّ وَلَا تُنظِرُونِ 71
{71} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake: Na wasomee kaumu yako "habari za Nuhu" katika kulingania kwake kaumu yake wakati alipowalingania kwa Mwenyezi Mungu muda mrefu, na akakaa kati yao miaka elfu moja isipokuwa miaka hamsini, lakini hakukuwazidishia kulingania kwake huko isipokuwa kuvuka mipaka. Kwa hivyo, wakachoka naye, na wakakata tamaa. Lakini yeye, rehema na amani ziwe juu yake, hakufanya uvivu wala hakuacha kuwalingania. Akawaambia, "Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu Ishara za Mwenyezi Mungu." Yaani, ikiwa kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu yale yatakayowafaa kwa ishara za Mwenyezi Mungu ambazo ni ushahidi ulio wazi na bainifu yamekuwa magumu juu yenu, na yakawa makubwa juu yenu na mnataka kunifikishia mabaya au kuikataa haki "basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu." Yaani, nimemtegemea Mwenyezi Mungu katika kuniondolea kila baya ninalokusudiwa kwalo, na kile ninachokilingania. Basi hili ndilo jeshi langu na silaha zangu. Nanyi basi leteni muwezayo yote miongoni mwa aina za silaha na idadi ya wasaidizi, "kisha likusanyeni jambo lenu pamoja" nyinyi nyote na asibaki nyuma yeyote miongoni mwenu na wala msiache chochote katika juhudi zenu. "Na" waleteni "washirika wenu" ambao mlikuwa mkiwaabudu na mnawafanya kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, "kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu." Yaani, msichanganyike katika hilo wala lisifichikane kwenu, bali na lidhihirike na liwe hadharani. "Kisha nihukumuni;" yaani, nihukumuni kwa adhabu na ubaya ambao uko katika uwezo wenu "wala msinipe muhula." Yaani, msinipe muhula wa saa moja katika mchana. Basi huu ni ushahidi wa uhakika na ishara kubwa juu ya usahihi wa ujumbe wake na ukweli wa kile alichokuja nacho. Kwa maana, alikuwa yeye peke yake bila ya ukoo wa kumlinda wala majeshi wa kumhifadhi. Na alikuwa amewashambulia kaumu wake kwa kupumbaza rai zao, kuweka wazi uharibifu wa dini yao, na kuwatia dosari miungu yao. Nao walikuwa wamebeba chuki na uadui juu yake ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko milima iliyo imara. Na pia walikuwa watu wenye uwezo na nguvu, naye akawaambia: Kusanyikeni nyinyi na washirika wenu na yeyote muwezaye, na wekeni wazi kila muwezalo miongoni mwa njama, kisha nifikishieni kama mnaweza kufanya hivyo; lakini hawakuweza kufanya lolote katika hayo. Kwa hivyo ikajulikana kwamba yeye ndiye mkweli kwa uhakika, nao ndio waongo katika yale wanayoyadai.