سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
سورت 10

Yunus

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 68

قَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۖ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ۖ لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ بِهَـٰذَآ ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ 68

{68} Yeye Mtukufu anasema akijulisha kuhusu uongo wa washirikina juu ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, "Walisema, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana." Basi akajitaka nafsi yake na hayo kwa kusema: "Ametakasika;" yaani, amesafika kutokana na yale wanayoyasema madhalimu katika kumnasibisha na mapungufu na ametukuka utukufu mkubwa. Kisha akaliwekea hilo hoja kadhaa: moja yake ni kauli yake, "Yeye ndiye asiyehitajia kitu." Yaani, kutohitaji kwote ni kwake, na aina mbalimbali za kutohitaji anazo yeye. Basi Yeye ndiye asiyehitaji ambako ni kutohitaji kukamilifu katika njia zote, na mazingatio yote, na kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, ikiwa yeye si mhitaji kwa njia yoyote ile, basi atajifanyia mwana kwa sababu gani? Je, ni kwa sababu ganianahitaji mwana? Basi hili linapingana na kutohitaji kwake. Kwa maana hajifanyii yeyote mwana isipokuwa kwa sababu ya upungufu katika kutohitaji kwake? Ushahidi wa pili ni kauli yake: "Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na hili ni neno la jumla, lenye kujumuisha. Hakitoki kwalo chochote kinachopatikana miongoni mwa wakazi wa mbinguni na ardhi. Vyote viliumbwa, na ni waja wanaomilikiwa. Na inavyojulikana ni kwamba sifa hii ya jumla inapingana na ukweli kwamba yeye ana mwana [miongoni mwao]. Kwa maana, mwana anakuwa wa aina sawa na mzazi wake, na hawi wa kuumbwa wala mmilikiwa. Kwa hivyo, kuvimiliki kwake vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi kwa ujumla kunapingana na kuwa kwavyo wana wake. Ushahidi wa tatu ni kauli yake "Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya!" Yaani, Je, mnayo hoja yoyote na ushahidi wowote unaoonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ana mwana? Na ikiwa wangelikuwa na ushahidi, basi wangeionyesha. Na alipowapa changamoto, na akawafanya washindwe kusimamisha ushahidi, ikajulikana ya kwamba yale wanayoyasema ni batili, na kwamba huko ni kusema bila ya elimu, na ndiyo maana akasema, "mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?" Kwani, haya ni miongoni mwa mambo makubwa yaliyoharamishwa.