Yunus
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ ٱلشَّمْسَ ضِيَآءً وَٱلْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُۥ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا۟ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ 5 إِنَّ فِى ٱخْتِلَـٰفِ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ 6
{5-6} Alipothibitisha umola wake na uungu wake, akataja ushahidi wa kiakili uliopo kwenye peo za macho zenye kuonyesha hili, na kuonyesha ukamilifu wake katika majina yake na sifa zake kama vile jua, mwezi, mbingu, ardhi, na vyote alivyoumba humo miongoni mwa viumbe wengine wote. Na akajulisha kuwa hizo ni Ishara “kwa kaumu wanaojua” na “kwa kaumu wamchao” kwa maana, Elimu huongoza kwenye kujua ushahidi ulio ndani yake, na jinsi ya kuondoa humo ushahidi kwa namna ya karibu zaidi. Na uchamungu husababisha matamanio ya heri katika moyo na kuhofu maovu, ambayo mawili haya yanatokana na ushahidi na hoja, elimu na yakini. Na muhtasari wa hayo ni kwamba uumbaji tu wa viumbe hawa kwa sifa hizi kunaonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na elimu yake, na uhai wake, na usimamia mambo yote wake, na uimara uliomo, na ustadi wake, na ubunifu mkubwa, na uzuri wake; yote yanaonyesha ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu. Na uzuri wa kuumba kwake, na upana wa elimu yake, na aina mbalimbali za manufaa na masilahi yaliyo ndani yake, kama vile kulifanya jua kuwa mwangaza, na mwezi kuwa nuru ambavyo kwavyo yanapatikana manufaa ya dharura na mengineyo yanayotokea, hayo yanaashiria rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na utunzaji wake kwa waja wake, na upana wa wema wake na ihsani yake. Na mambo maalumu yaliyomo yanaashiria mapenzi ya Mwenyezi Mungu na matashi yake yatekelezekanayo. Na hilo linaonyesha kwamba Yeye pekee ndiye Muabudiwa, Mpendwa, Msifiwa, Mwenye utukufu, heshima, na sifa kuu kuu, ambaye haifai kumtaka mwingine wala kumhofu isipokuwa Yeye, wala haifai kumfanyia dua safi isipokuwa Yeye. Si mwingineye miongoni mwa viumbe wanaolelewa, wanaomhitaji Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote. Na katika aya hizi kuna kuhimiza na kutia moyo juu ya kutafakari viumbe vya Mwenyezi Mungu na kuwatazama kwa jicho la kuzingatia. Kwa maana kupitia hayo, utambuzi unakuwa mpana, na inazidi imani na akili, na maumbile yanaimarika. Na katika kupuuza hilo kuna kuyapuuza yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha, na kufunga kuongezeka kwa imani, na kudumaa kwa akili na maumbile.