At-Tawba
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
ٱلَّذِينَ يَلْمِزُونَ ٱلْمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ فِى ٱلصَّدَقَـٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ ۙ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ 79
{79} Na hii pia ni miongoni mwa fedheha za waaafiki. Kwani walikuwa - Mwenyezi Mungu awatie mbali na rehema - hawaachi kitu katika mambo yoyote ya Uislamu, na Waislamu wanachoweza kusema kitu kuhusiana nacho, isipokuwa walisema na kuzua uwongo kwa dhuluma na kuvuka mipaka. Basi Mwenyezi Mungu na Mtume wake walipohimiza juu ya sadaka, Waislamu wakaharakisha kufanya hivyo, na wakatoa katika mali zao, kila mmoja kwa hali yake, baadhi yao walikuwa na vingi na baadhi yao walikuwa na kidogo. Kwa hivyo, wakawabeua waliotoa vingi miongoni mwao kwa kusema kwamba makusudio yake katika kutoa kwake ni kujionyesha na kutaka sifa. Na wakamwambia aliyetoa kichache, fukara: Hakika Mwenyezi Mungu hahitaji sadaka ya huyu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Wale wanaowabeua," yaani, wanaowatia dosari na kuwashutumu "Waumini wanaotoa sadaka nyingi." Wakasema: hawa wanajionyesha, makusudio yao ni kujifahirisha, na kujionyesha "na" wanawabeua "wasio nacho cha kutoa ila kiasi cha juhudi yao" na wanatoa kile wawezacho. Kwa hivyo wanawaambia: Mwenyezi Mungu hahitaji sadaka zenu, "hivyo wanawafanyia masikhara." Basi Mwenyezi Mungu akawalipa juu ya vitendo vyao hivyo kwa kuwafanyia maskhara. "Nao wana adhabu chungu!" Kwa maana walikusanya katika maneno yao haya makatazo kadhaa: Miongoni mwake ni kufuatilia kwao hali za Waumini, na kuwania kwao sana ili wapate maneno ya kusema juu yao. Na Mwenyezi Mungu anasema, "Hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa wale walioamini, wana adhabu chungu katika dunia na Akhera." Na miongoni mwake ni kushutumu kwao waumini kwa sababu ya imani yao, huku wakimkufuru Mwenyezi Mungu na kuichukia dini yake. Na miongoni mwake ni kwamba, kubeua ni haramu, bali ni katika madhambi makubwa katika mambo ya dunia. Na ama kubeua katika mambo ya utiifu, basi ni kubaya, na kubaya zaidi. Na miongoni mwake ni kwamba, mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akajitolea kwa sifa mojawapo ya sifa za heri, basi kile kinachopaswa ni kumsaidia na kumkakamua juu ya kufanya hivyo. Nao hawa walikusudia kuwazuia kwa yale waliyoyasema juu yao, na kuwashutumu juu yake. Na miongoni mwake ni kwamba, kuhukumu kwao yule aliyetoa mali nyingi kwamba ni mwenye kujionyesha ni kosa kubwa, na kuhukumu mambo ya ghaibu, na kutuhumu kwa mujibu wa dhana tu. Basi je, ni uovu gani mkubwa zaidi kuliko huu? Na miongoni mwake ni kwamba kusema kwao kuhusu mwenye kutoa sadaka kidogo, "Mwenyezi Mungu hahitaji sadaka ya huyu!" Ni maneno ambayo makusudio yake ni batili kwani Mwenyezi Mungu hahitaji sadaka ya mwenye kutoa sadaka kidogo na mwenye kutoa sadaka nyingi, bali hawahitaji wakazi wa mbingu zote na wa ardhi, lakini Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamrisha waja wake kufanya yale wanayoyahitaji wao. Kwa maana Mwenyezi Mungu hata kama si mhitaji wa hayo, wao wanayahitaji. "Kwa hivyo, anayetenda chembe ya wema, atauona!" Na katika usemi huu kuna jambo la kuzuia heri ambalo liko dhahiri na wazi. Na ndiyo maana yakawa malipo yao ni kuwa Mwenyezi Mungu atawafanyia masihara, "Nao wana adhabu chungu!"