At-Tawba
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْأَحْبَارِ وَٱلرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلْبَـٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۗ وَٱلَّذِينَ يَكْنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ 34
{34} Hili ni tahadharisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake Waumini juu ya wengi katika makuhani na wamonaki. Yaani, wanazuoni na waja ambao wanakula mali za watu kwa batili. Yaani, bila ya haki, na wanazuilia njia ya Mwenyezi Mungu; kwani kama wana mishahara kutoka katika mali za watu, au watu wakawapa kutoka kwa mali zao, basi hilo ni kwa sababu ya elimu yao na ibada yao, na ni kwa sababu ya uwongofu wao na kuongoza kwao. Na hawa wanazichukua na wanazuilia watu njia ya Mwenyezi Mungu, basi inakuwa kuzichukua kwao kwa Njia hii ni haramu na dhuluma. Kwa maana watu hawakuzitoa wakawapa kutoka kwa mali zao isipokuwa ili wawaonyeshe njia iliyonyooka. Na katika kuchukua kwao katika mali za watu bila ya haki ni kwamba wawape ili wawatolee hukumu ya suala fulani la kidini (Fatwa) au wawahukumie kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremsha. Kwa hivyo, makuhani hawa na wamonaki naitahadhariwe kwayo mambo mawili haya: kuchukua kwao kwa mali za watu bila ya haki, na kuzuilia kwao watu njia ya Mwenyezi Mungu. "Na wale wanaolimbika dhahabu na fedha;" yaani, wanazishikilia, "wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu." Yaani, njia za heri zifikishazo kwa Mwenyezi Mungu. Na huku ndiko kulimbika kulikoharamishwa. Kuishikilia mali na kuacha kutoa kwa ajili ya matumizi ya wajibu, kama vile kuzuia Zaka kutoka humo au matumizi ya lazima ya mke au jamaa au matumizi katika njia ya Mwenyezi Mungu ikiwa ni wajibu; "basi wabashirie adhabu chungu."