Al-Muddaththir
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
كُلُّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ 38 إِلَّآ أَصْحَـٰبَ ٱلْيَمِينِ 39 فِى جَنَّـٰتٍ يَتَسَآءَلُونَ 40 عَنِ ٱلْمُجْرِمِينَ 41 مَا سَلَكَكُمْ فِى سَقَرَ 42 قَالُوا۟ لَمْ نَكُ مِنَ ٱلْمُصَلِّينَ 43 وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ ٱلْمِسْكِينَ 44 وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلْخَآئِضِينَ 45 وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ 46 حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلْيَقِينُ 47 فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَـٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ 48
{38 - 48} "Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma" miongoni mwa vitendo viovu na vibaya. Vimefungwa shingoni kwake sawasawa na vikamfanya kustahiki kuadhibiwa kwavyo. "Isipokuwa watu wa kuliani" kwani hawakushikwa rahanini. Bali walifunguliwa huru na wakafurahishwa. "Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana habari za wakosefu." Humo watakuwa wamepewa yote waliyoyataka na itawatimia starehe na utulivu, mpaka wakaelekeana kuulizana maswali, kisha mazungumzo hayo yakawapelekea kuuliza juu ya wahalifu. Walifikia hali gani? Je, walipata kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi? Kisha baadhi yao wakaambiana: 'Je, mnawaona?' Basi wakawatazama na wakawaona katikati ya Jahannamu wakiteswa, kwa hivyo wakawaambia: “Ni nini kilichokupelekeni Saqr?” Wakasema: "Hatukuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini." Kwa hivyo hawakumkusudia mwabudiwa peke yake, wala hawakuwa wakiwafanyia wema na kuwanufaisha viumbe wahitaji. "Na tulikuwa tukizama pamoja na wale waliozama katika maovu" tukiijadili na kuipinga haki kwayo. "Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo." Hizi ndizo athari za kujizamisha katika batili, ambazo ni kukadhibisha haki. Na katika haki kubwa zaidi ni kuamini katika siku ya malipo, ambayo ndiyo siku ya malipo juu ya matendo na kudhihiri ufalme wa Mwenyezi Mungu na hukumu yake ya uadilifu kwa viumbe vyote. Basi sisi tukaendelea kufanya matendo kulingana na dhehebu hili batili. "Mpaka yakini ilipotufikia." Yaani, mauti. Basi walipokufia katika ukafiri, wakakosa hila yoyote, na mlango wa matumaini ukafungika mbele ya nyuso zao. "Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi." Kwa sababu hawamfanyii uombezi yeyote isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemridhia. Na hao, Mwenyezi Mungu hayaridhii matendo yao.