İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qalam
Sure 68

Al-Qalam

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 4

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ 4

{4} Ndiyo maana akasema: "Na hakika wewe una tabia tukufu." Yaani, umeinuka juu kwa tabia hizo ambazo Mwenyezi Mungu alikuneemesha kwazo. Na jumla ya tabia zake tukufu ni yale aliyoyafasiri mama wa Waumini, Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alipowambia wale waliomuuliza kumhusu yeye, akasema: 'Tabia yake ilikuwa ni Qur-ani.' Haya ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majahili." Na pia akasema, "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao..." hadi mwisho wa aya hii. Na pia akasema, "Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayokutaabisheni..." hadi mwisho wa Aya hii, na pia Aya zingine mfano wa hizi zinazoashiria kusifika kwake - yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na tabia njema na aya zinazohimiza kila tabia nzuri. Basi yeye akawa anasifika kwa kamilizi zake zaidi na tukufu zake zaidi. Naye katika kila< kipengele katika hizo alikuwa katika kilele cha juu kabisa. Alikuwa mwepesi, laini na karibu sana kwa watu, mwenye kuitikia mwito wa anayemwita, mwenye kutimiza mahitaji ya wale wanaotafuta awakidhie mahitaji yao, mwenye kuliwaza moyo wa anayemwomba, hakuwa akimnyima wala kumrudisha patupu. Na ikiwa maswahaba zake walitaka kitu kutoka kwake; alikuwa akiafikiana nao juu yake na kuwafuata ndani yake ikiwa halina ubaya wowote ndani yake. Na akiazimia kufanya jambo, hakuwapa kisogo bila ya kuwahusisha. Bali alikuwa akishauriana nao na kutaka maoni yao kuhusiana nalo. Na alikuwa akikubali kutoka kwa mtenda mazuri wao, na anamsamehe mtenda mabaya wao, na wala hakuwa akitangamana na anyekaa naye isipokuwa kwa kukaa naye kwa njia kamilifu na nzuri zaidi. Alikuwa hamkunjii uso wake, wala kumfanyia ukali katika kuzungumza naye, wala haachi kumfanyia bashasha kwa sababu ya uovu wake, wala kumshikilia kwa sababu ya kasoro za ulimi wake, wala hamchukulii ubaya kwa sababu ya ugumu anaomfanyia. Bali alikuwa akimtendea wema wa hali ya juu sana, na kumvumilia kwa ustahimilivu wa hali ya juu sana - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.