Al-An'aam
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَذَرِ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِۦٓ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌۢ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِىٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَآ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أُبْسِلُوا۟ بِمَا كَسَبُوا۟ ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ 70
{70} Kinachokusudiwa kwa waja ni kuwa na ikhlasi kwa mwenyezi Mungu katika dini kwa kumwabudu Yeye pekee, bila mshirika yeyote, na wafanye wawezalo ili kumridhisha Yeye na kumpenda. Na hilo linajumuisha moyo kuja kwa Mwenyezi Mungu na kumuelekea, na kwamba juhudi ya mja iwe yenye manufaa, na yenye bidii na si ya mzaha, na ikhlasi kwa uso wa Mwenyezi Mungu na siyo kwa kujionyesha wala kusifiwa. Na hii ndiyo Dini ya hakika ambayo inasemwa; Dini. Ama mwenye kudai kuwa yuko katika haki, na kwamba yeye ni mwenye dini na uchamungu, na ilhali aliifanya dini yake kuwa ni mchezo na pumbao, kwa kuwa moyo wake ulifanya pumbao ukaacha kumpenda mwenyezi mungu na kumjua. Na akayajia kila yenye kumdhuru, na akafanya pumbao katika batili yake, na akacheza ndani yake kwa mwili wake. Kwa sababu matendo na juhudi ikiwa ni kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hayo ni mchezo. Na kwa sababu hii Mwenyezi Mungu mtukufu akaamrisha ya kwamba aachwe, na atahadhariwe, na wala mtu asidanganywe naye; na iangaliwe hali yake, na mtu ajitahadhari na matendo yake; na wala asidanganywe na kuzuia kwake yale yenye kumuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu. "Nawe kumbusha kwayo;" yaani, kumbusha kwa Qur-aani yale yenye kuwanufaisha waja kwa amri na kwa undani, na kwa kuiboresha kwa kutaja yale yaliyomo ya sifa nzuri nzuri, na yale yanayowadhuru waja kwa kuyakataza, na kubainisha kwa undani aina zake, na kubainisha yale yaliyomo ya sifa mbaya, mbovu zenye kuitia kuyaacha. Na yote haya ni ili nafsi yoyote ile isiangamizwe kwa yale iliyoyachuma. Yaani, kabla mja hajaingia katika madhambi na kumfanyia ujasiri Mwenye kuyajua vyema ya ghaibu na kuendelea kwake kufanya hayo yanayohofisha. Kwa hivyo ikumbushe na ipe mawaidha ili ijizuie, na ikomeke, na iache kuyafanya. Na kauli yake, "hali ya kuwa haina kando na Mwenyezi Mungu, mlinzi yeyote wala mwombezi." Yaani kabla ya kumzunguka madhambi yake, kisha hakuna hata mmoja katika viumbe atakayeinufaisha, si jamaa wala rafiki, na wala hakuna wa kuisimamia kando na Mwenyezi Mungu yeyote wala mwombezi wa kuiombea. "Na hata ikitoa kila fidia;" yaani, ikitoa kila fidia, hata kama ni kwa dhahabu ya ujazo wa ardhi, "haitakubaliwa kutoka kwake." Yaani, haitakubalika wala haitafaa. "Hao," walioelezwa kuwa yale yaliyotajwa, "ndio walioangamizwa;" na wakakata tamaa ya heri yoyote. Na hayo ni "kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao wana kinywaji cha maji ya moto kabisa." Yaani, maji ya moto ambayo joto lake linafikia kubambua nyuso zao na kuyakata matumbo yao; "na adhabu chungu kwa yale waliyokuwa wakikufuru."