Al-Waaqia
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَأَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ 27 فِى سِدْرٍ مَّخْضُودٍ 28 وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ 29 وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ 30 وَمَآءٍ مَّسْكُوبٍ 31 وَفَـٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ 32 لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ 33 وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ 34
{27 - 34} Kisha akataja aliyowaandalia watu wa kuliani, akasema: "Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?" Yaani, jambo lao ni kuu na hali yao kubwa. "Katika mikunazi isiyo na miba" wala matawi mabaya, yenye madhara ndani yake, na matunda mazuri yameekwa mahali pa matawi hayo. Mti huu wa mkunazi ni katika miti maalumu yenye kivuli cha kufunika mno na pia mwili hupata raha ndani yake. "Na migomba iliyopangiliwa" Mti huu mkubwa unapatikana jangwani ambao matawi yake hujipanga kwa matunda matamu ya kuvutia. "Na maji yanayomiminika" kwa wingi kutoka katika chemichemi na mito ipitayo "na matunda mengi. Hayatindikii wala hayakatazwi." Yaani, si katika cheo kimoja na matunda ya duniani; ambayo hayapatikani katika wakati fulani na inakuwa haiwezekani na ni vigumu kwa mwenye kuyatafuta. Bali hayo yanapatikana siku zote, na matunda yake yako karibu na mja, anaweza kuyachukua hata awe katika hali gani. "Na matandiko yaliyonyanyuliwa" juu ya vitanda kwa urefu mkubwa, na magodoro hayo yametengenezwa kwa hariri, dhahabu, lulu, na yale ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anajua.