Al-Qamar
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا۟ عَبْدَنَا وَقَالُوا۟ مَجْنُونٌ وَٱزْدُجِرَ 9
{9} Alipotaja Mwenyezi Mungu Mwenye baraka nyingi, Mtukufu hali ya wale waliomkadhibisha Mtume wake, na kwamba ishara haziwaingii kitu wala haziwanufaishi chochote, akawaonya na kuwaogopesha kwa adhabu za umma wa zamani waliowakadhibisha Mitume, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaangamiza na kuwaletea adhabu yake. Basi akawataja watu wa Nuhu, ambaye alikuwa Mtume wa kwanza ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa watu wanaoabudu masanamu. Akawalingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumwabudu Yeye peke yake bila mshirika, lakini wakasema: "Kamwe msiwaache miungu yenu, wala kamwe msimwache Wadda, wala Suwaa', wala Yaghutha, wala Yau'qa wala Nasra.” Naye Nuhu akaendelea kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa siri, mchana na usiku. Lakini, hilo halikuwazidishia isipokuwa kuwa na ukaidi, kupindukia mipaka na kumkashifu Nabii wao. Ndiyo maana akasema hapa: "Wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu." Kwa sababu ya madai yao ya kwamba yale ambayo wao na baba zao wanayaamini ya ushirikina na upotofu ndiyo yanayoashiriwa na akili timamu, na kwamba yale ambayo Nuhu, amani iwe juu yake, alikuja nayo ni ujinga na upotofu ambao hauwezi kutokea isipokuwa kwa wendawazimu, lakini walidanganya katika hilo, na wakapindua mambo ya uhakika yaliyothibiti kisheria na kiakili. Kwani, aliyokuja nayo ndiyo haki iliyo dhabiti isiyobadilika inayoongoza akili angavu na nyoofu kwenye uwongofu, nuru na uwongofu. Ilhali hayo wanayoyafanya ni ujinga na upotofu ulio wazi. Na kauli yake: "Na akakaripiwa." Yaani, watu wake walimkemea na kumkaripia pale alipowaita kwa Mwenyezi Mungu, na tena haikuwatosha - Mwenyezi Mungu awaangamize – kutomwamini kwao wala kumkadhibisha kwao. Bali pia walimfikishia udhia namna walivyoweza. Na hivyo ndivyo walivyo maadui wote wa Mitume. Walikuwa wakiwafanyia hivi tu Mitume wao.