İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Qaaf
Sure 50

Qaaf

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 2

بَلْ عَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا شَىْءٌ عَجِيبٌ 2

{2} Hili linalazimu kuifuata kikamilifu, kutekeleza mambo yake haraka, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya kutupa Qur-ani hii, lakini watu wengi hawazithamini neema za Mwenyezi Mungu kama zinavyostahiki, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Bali wanastaajabu." Yaani wale waliomkadhibisha Mtume – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – "kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao" ili awaonye dhidi ya mambo yatakayowadhuru na awaamrishe yale yatakayowafaa, naye ni wa aina sawa nao, ambaye wanaweza kujifunza kutoka kwake na kujua hali zake na ukweli wake, kwa hivyo wakastaajabia jambo ambalo hawapaswi kulistaajabia. Bali inastaajabiwa akili ya mwenye kustaajabishwa na hilo. "Na wakasema makafiri" ambao walifanywa na ukafiri wao na kukadhibisha kwao si kwa sababu ya kuwa na upungufu katika werevu wao na maoni yao: "Hili ni jambo la ajabu!" Katika mshangao wao huu, wako baina ya vitu viwili: ima ni wakweli katika mshangao wao huo. Na hili linaashiria ujinga wao wa hali ya juu na udhaifu wa akili zao. Wako kama mwendawazimu ambaye anashangazwa na maneno ya mtu mwenye akili timamu, na wako kama mwoga anayeshangazwa na wapiganaji hodari wanapokutana na wapiganaji wengine hodari, na ni kama bahili anayeshangazwa na ukarimu wa watu wakarimu. Ni madhara gani yatakayotokea kwa sababu ya kushangaa kwa mtu ambaye hii ndiyo hali yake? Je, kustaajabu kwake huku si isipokuwa ushahidi juu ya kuongezeka kwa ujinga na dhuluma yake? Na ima wanashangazwa kwa namna ambayo tayari wanajua makosa yao katika hilo. Basi hii ndiyo dhuluma kubwa na mbaya kabisa.