Az-Zukhruf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَهُوَ ٱلَّذِى فِى ٱلسَّمَآءِ إِلَـٰهٌ وَفِى ٱلْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ 84
{84} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa Yeye peke yake ndiye anayefaa kufanyiwa uungu na kuabidiwa mbinguni na ardhini, kwa hivyo wakaazi wote wa mbinguni, na Waumini miongoni mwa wakazi wa ardhini wanamuabudu Yeye na wanampa taadhima na wananyenyekea chini ya utukufu wake na wanahitaji mno ukamilifu wake. "Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake." "Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake." "Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake." Basi Yeye Mtukufu ndiye anayefanyiwa uungu, anayeabudiwa na viumbe vyote, kwa kutii na kwa kutotaka. Na hii ni kama kauli yake Mtukufu: "Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini." Yaani: Uungu wake na upendo wake vimo ndani ya viwili hivyo, na ama Yeye, ameinuka juu ya kiti chake cha enzi, bali na viumbe vyake, amepwekeka kwa utukufu wake, ametukuka kwa ukamilifu wake. "Naye ndiye Mwenye hekima" ambaye amefanya vilivyo kila alichokiumba, na akafanya sawasawa alichokiweka kuwa sheria. Kwa hivyo, hakuumba chochote ila kwa ajili ya hekima fulani, na hakutunga sheria yoyote isipokuwa kwa hekima fulani. Na hukumu yake ya kimajaaliwa, ya kisheria na ya kimalipo zinajumuisha hekima. "Ajuaye zaidi" kila kitu. Anajua siri na mambo yaliyofichika zaidi, na wala hakifichikani kwake chenye uzito hata wa chembe katika ulimwengu wa juu wala wa chini, wala kidogo zaidi kuliko hicho wala kikubwa zaidi.