An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلْيَخْشَ ٱلَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا۟ مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَـٰفًا خَافُوا۟ عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلْيَقُولُوا۟ قَوْلًا سَدِيدًا 9
{9} Ilisemwa kuwa haya anaambiwa yule ambaye amemhudhuria yule ambaye amejiwa na kifo, na ambaye ni dhalimu katika wasia wake, kwamba amwamuru afanye uadilifu katika wasia wake na usawa ndani yake, kwa ushahidi wa kauli yake, “na waseme kauli iliyo sawa.” Yani, iliyo sawa inayoafikiana na uadilifu na ada. Na kwamba wamwamrishe yule anayetaka kuwausia watoto wake kwa kile wanachopenda wafanyiwe watoto wao baada yao. Na ilisemwa kuwa kilichokusudiwa kwa hilo walezi wa wale wasioweza kufanya uamuzi wa busara kama vile wendawazimu, na watoto wadogo, na walio dhaifu kwamba wawatendee katika masilahi yao ya kidini na ya kidunia kama wanavyopenda watendewe dhuria wao wadhaifu baada yao. “Na wamche Mwenyezi Mungu,” yani, katika ulezi wao juu wengine. Yani wawatendee yale ambayo uchamungu ndani yake kama vile kutowadunisha, kuwasimamia, na kuwafanya wamche Mwenyezi Mungu.