İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sure 4

An-Nisaa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 74

فَلْيُقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يَشْرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا بِٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا 74

{74} Na katika upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kwamba asiwakatie rehema yake, wala asiwafungie milango yake. Bali mwenye kufanya kile kisichofaa, anamwamrisha na kumwita ili atengeneze mapungufu yake na akamilishe nafsi yake. Ndiyo maana akawaamrisha hawa wamkusudie Yeye tu na watoke waende katika njia yake. Akasema, “Basi na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanauza uhai wa dunia kwa Akhera.” Hii ni moja ya kauli kuhusiana na Aya hii, nayo ndiyo sahihi yake zaidi. Na ikasemwa kuwa maana yake ni kwamba na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu Waumini wenye imani kamili walio wakweli katika Imani yao. “Ambao wanauza uhai wa dunia kwa Akhera.” Yani wanaiuza dunia kwa sababu ya kutoitaka kwa Akhera kwa sababu ya kuitaka. Kwa maana hawa ndio ambao wanaongeleshwa, kwa sababu wao ndio walizitayarisha nafsi zao na wakazizoesha kupigana Jihadi dhidi ya maadui, kwa sababu ya kile walicho nacho cha imani kamili inayolazimu hilo. Na wale wanaojikokota, basi hawajalishi, watoke au wakae. Na hii inakuwa sawa na kauli yake Yeye Mtukufu, “Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika, wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu,” mpaka mwisho wa Aya. Na kauli yake, “Na ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasioyakataa.” Na ikasemwa: hakika maana ya Aya hii ni: Basi naapigane mpiganaji vita na mwenye kufanya jitihada dhidi ya makafiri ambao wanaununua uhai wa dunia kwa Akhera. Kwa hivyo, ikiwa maana yake ni hiyo, inakuwa kauli yake “ambao” katika nafasi ya mtendwa. “Na mwenye kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu,” yani katika Jihadi aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mja awe anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, akiukusudia uso wa Mwenyezi Mungu. “Kisha akauwawa au akashinda, basi tutampa ujira mkubwa” kama ziada juu ya imani yake, na dini yake, na ngawira, na sifa nzuri, na thawabu za wanaopambana katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ambao Mwenyezi Mungu aliwaandalia ndani ya Pepo yale ambayo hakuna jicho liliwahi kuyaona, wala hakuna sikio liliwahi kuyasikia, wala hayakuwahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote.