An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَٱلْمُحْصَنَـٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ ۖ كِتَـٰبَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا۟ بِأَمْوَٰلِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَـٰفِحِينَ ۚ فَمَا ٱسْتَمْتَعْتُم بِهِۦ مِنْهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَٰضَيْتُم بِهِۦ مِنۢ بَعْدِ ٱلْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا 24
{24} Na miongoni mwa wale walioharamishwa katika ndoa ni "wanawake wenye waume." Kwani ni haramu kuwaoa maadamu wako chini ya ulinzi wa mume, mpaka apewe talaka na imalizike eda yake. "Isipokuwa wale waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia." Yani, kwa kutekwa katika vita. Basi mwanamke kafiri mwenye mume atakapotekwa, anakuwa halali kwa Waislamu baada ya kubainika utupu wa tumbo lake la uzazi. Lakini ikiwa mkajaki aliyeolewa atakapouzwa au akipeanwa kama zawadi, basi ndoa yake haibatiliki. Kwa sababu mmiliki wa pili alishuka kwenye nafasi ya yule wa kwanza. Na kwa sababu ya hadithi ya Barira wakati Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -alipompa chaguo. Na kauli yake, "Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu." Yani, shikamaneni nacho na ongokeni kwacho. Kwani, ndani yake kuna uponyaji na nuru. Na ndani yake kuna kubainisha kwa kina yale yanayoruhusiwa na yale yaliyoharamishwa. Na aliingia katika kauli yake, "Na mmehalalishiwa wasio kuwa hao" kila ambaye hakutajwa katika Aya hii, basi yeye ni halali na ni nzuri. Kwa hivyo, haramu imefungiwa, nayo halali haina kikomo au kizuizi; kwa sababu ya upole kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na rehema, na urahisishaji kwa waja. Na kauli yake, "mtafute kwa mali yenu." Yani mtafute yule ambaye macho yenu yamemuona na chaguo lenu katika wale wanawake ambao Mwenyezi Mungu amewaruhusu hali ya kuwa ni "kwa kuoa." Yani, kujiweka mbali na zinaa, na mnawaweka wake zenu mbali nayo pia, "pasi na kuzini." Na safah ni kumwaga maji katika halali na katika haramu. Na mwenye kufanya hilo hamlindi mke wake. Kwa sababu, aliweka matamanio yake katika haramu, kwa hivyo linadhoofika lenye kumuita kwenye halali. Hivyo basi, habaki kuwa ni mwenye kumlinda mkewe. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba watu wasiokuwa safi hawaozwi, kwa kauli yake Yeye Mtukufu, "Mwanamume mzinifu hamwoi isipokuwa mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamume mzinifu au mshirikina." "Kama mnavyostarehe nao" yani yule mliyemuoa. "Basi wapeni mahari yao," yani, malipo kwa kubadilishana na starehe. Na ndiyo maana mume akimwingilia mkewe, inathibiti ampe mahari yake kwa kuwa "ni wajibu." Yani kuwapa kwenu malipo yao ni faradhi ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka juu yenu, na si sawa na sadaka ambayo akitaka, anaitekeleza, na akitaka anaikataa. Au maana ya kauli yake, "ni wajibu" yani yameshapimwa. Yani mmeshayapima, na yakawa wajibu juu yenu. Kwa hivyo msipunguze chochote kwayo. "Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakachokubaliana baada ya kutimiza wajibu." Yani kwa kuiongeza kutoka kwa mume au kuiachilia mbali kutoka kwa mke kwa kuridhia na roho nafsi. Hii ndiyo kauli ya wengi wa wafasiri. Na wengi wao walisema: Iliteremka kuhusu kustarehe na wanawake kwa muda, ambako kulikuwa halali mwanzoni mwa Uislamu, kisha Nabii -rehema na amani zimshukie -akakuharamisha. Na kwamba kabla ya kufanywa haramu, ilikuwa ameamrishwa kumkamilishia muda na kumpa malipo yake. Kisha muda huu baina yao unapokwisha na wakaafikiana baada ya kuwekeana kiwango maalumu cha mahari, hakuna lawama juu yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. "Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima." Yani ni mwenye elimu kamili na hekima kamili. Na katika elimu yake na hekima yake ni kwamba aliwawekea sheria hizi, na akawawekea mipaka hii inayotenganisha yaliyo halali na haramu. Kisha Yeye Mtukufu akasema: