As-Saaffaat
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ 75 وَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ 76 وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ 77 وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ 78 سَلَـٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِى ٱلْعَـٰلَمِينَ 79 إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ 80 إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ 81 ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ 82
Kisha akataja mfano wa mwisho wa mataifa waliokadhibisha, akasema:
{75 - 82} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu mja wake na Mtume wake, Nuhu, amani iwe juu yake, Mitume wa kwanza, kwamba alipowalingania watu wake kwa Mwenyezi Mungu kwa muda huo mrefu, lakini wito wake haukuwazidisha isipokuwa kukimbia; kwamba akamwomba Mola wake Mlezi na akasema: "Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri..." hadi mwisho wa aya. Na akasema: "Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na watu mafisadi hawa!" Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia. Na Mwenyezi Mungu akajisifu, akasema: "Na Sisi ni bora wa waitikiaji" dua za waombaji na kusikia dua zao na unyenyekevu wao kwetu. Basi Mwenyezi Mungu akamjibu kwa jawabu linalolingana na alivyoomba. Alimuokoa yeye na familia yake kutokana na msiba mkubwa, akawazamisha makafiri wote, na akakibakisha kizazi chake na kizazi kikaendelea kuzaana mfululizo. Basi watu wote ni kizazi cha Nuhu, amani imshukie. Na pia akamjaalia sifa njema zinazoendelea mpaka zama za watu wa mwisho, kwa sababu alikuwa mwema katika kumuabudu Muumba, mwema kwa viumbe. Hii ndiyo desturi yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusiana na wanaofanya wema; kuwaenezea sifa njema kulingana na wema wao. Na kauli yake: "Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini," inaashiria kuwa imani ndiyo daraja ya juu kabisa ya ibada na kwamba inajumuisha sheria zote za Dini, misingi yake na matawi yake,kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwasifu kwayo waja wake maalumu.