Faatir
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَمِنَ ٱلنَّاسِ وَٱلدَّوَآبِّ وَٱلْأَنْعَـٰمِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ كَذَٰلِكَ ۗ إِنَّمَا يَخْشَى ٱللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ ٱلْعُلَمَـٰٓؤُا۟ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ 28
28. Na katika hayo ni wamo watu, na wanyama, na mifugo. Ndani yao kuna tofauti katika rangi zao, sifa zao, sauti zao na mionekano yao inayoonekana kwa macho na kushuhudiwa na watazamaji, na vyote hivyo vilitokana na asili moja na kiini kimoja. Kwa hivyo, kutofautiana kwao huku ni ushahidi wa kiakili juu ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ambayo yalivifanya maalumu vitu hivyo kwa kuvipa kila kimoja rangi yake na sifa zake, na pia ni ishara juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu ambapo aliviumba hivyo. Na pia ni ishara juu ya hekima yake na rehema zake ambapo tofauti hizo zina masilahi, manufaa, na kujua njia na watu kujuana wao kwa wao kama inavyojulikana. Haya ni ushahidi juu ya upana wa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba atawafufua waliomo makaburini. Lakini mtu aliyeghafilika huyatazama mambo haya na mengineyo kwa mtazamo wa kughafilika ambako hakumfanyi kukumbuka. Wale wanaofaidika nayo ni wale wanaomcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na ambao wanajua kwa fikira zao sahihi hekima iliyoko ndani yake, na ndiyo maana akasema: "Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni." Kwa hivyo, kila ambaye anamjua vyema Mwenyezi Mungu, anakuwa ni mwenye kumuogopa zaidi, na huku kumhofu Mwenyezi Mungu kunamfanya ajiepushe na dhambi na kujitayarisha kukutana na yule anayemcha.Na huu ni ushahidi wa ubora wa elimu,kwani inaitia kumcha Mwenyezi Mungu. Na wale wanaomcha ndio watakaopata utukufu wake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wako radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi." "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu" kamili. Na katika nguvu zake ni kuumba kwake viumbe hawa walio kinyume. "Mwenye kusamehe" dhambi za waliotubu.