İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hajj
Sure 22

Al-Hajj

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 14

إِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ 14

{14} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtaja mwenye kubishana kwa uwongo, na kwamba yeye ni wa aina mbili: mwigaji na mwenye kupinga. Ametaja kuwa mwenye sifa ya imani pia amegawanyika katika makundi mawili; kundi ambalo imani haijaingia moyoni mwake, kama ilivyotajwa hapo juu. Na kundi la pili: Muumini wa kweli. Imani yake juu ya matendo mema ilikuwa ya kweli, hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia kuwa atawaingiza katika "Bustani zipitazo mito kati yake:" Pepo iliitwa bustani kwa sababu ilikuwa na majumba, na makasri, na miti na mimea inayowafanya waliomo humo wajifiche na wasionekane kwa sababu ya wingi wake. "Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo:" Kwa hivyo chochote anachotaka Mwenyezi Mungu; hukifanya hivyo; bila pingamizi wala upinzani, ikiwa ni pamoja na kuwaleta watu wa Peponi humo. Mwenyezi Mungu alitufanya sisi kuwa miongoni mwao kwa neema na ukarimu wake.