Al-Baqara
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَمَآ أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُهُۥ ۗ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ 270 إِن تُبْدُوا۟ ٱلصَّدَقَـٰتِ فَنِعِمَّا هِىَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا ٱلْفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمْ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ 271
{270 - 271} Mola Mtukufu anajulisha kwamba chochote watoacho cha matumizi wenye kutoa, au sadaka watoayo wenye kutoa sadaka, au nadhiri wawekayo wenye kuweka nadhiri; basi hakika Mwenyezi Mungu anajua hilo. Na maudhui ya kujulisha kuhusu elimu yake yanaashiria malipo. Na kwamba Mwenyezi Mungu haupotei uzito wa chembe kwake. Na anajua nia gani nzuri au mbaya iliyotoka kwake. Na kwamba madhalimu wanaozuia yale aliyowawajibishia Mwenyezi Mungu au wanaoingia katika yale aliyowaharamishia; wao hawana kando na Yeye wasaidizi wowote wa kuwasaidia na kuwazuia. Na kwamba ni lazima adhabu ziwashukie. Na alijulisha kwamba ikiwa mwenye kutoa sadaka akiidhihirisha, basi hiyo ni bora. Na akiificha na akaikabidhi kwa fakiri, basi linakuwa bora zadi. Kwa sababu, kumpa masikini kwa kuficha ni wema mwingine. Na pia inaonyesha nguvu ya ikhlasi. Na mmoja wa wale saba ambao Mwenyezi Mungu atawatia katika kivuli chake, ni yule anayetoa sadaka na akaificha; mpaka mkono wake wa kushoto hukujua kile ambacho mkono wake wa kulia ulitoa. Na katika kauli yake: "Na mkiificha na mkawapa mafakiri kwa siri, basi hivyo ni heri kwenu," kuna faida nzuri. Nayo ni kwamba ukimpa fakiri, kuificha (sadaka) ni bora kuliko kuidhihirisha . Lakini ikiwa itatumika katika mradi wa hisani, basi hakuna katika aya chenye kuonyesha ubora katika kukificha. Bali, hapa misingi ya sheria inaonyesha kuzingatia masilahi. Kwa maana, pengine kuidhihirisha kukawa bora ili kuwe kielelezo na kuhamasisha nafsi juu ya kufanya matendo mema. Na kauli yake: "Na atawafutia katika maovu yenu." Kuna kwamba katika sadaka yanajumuika mambo mawili ndani yake: Kupatikana kwa heri, ambayo ni wingi wa mema na thawabu na malipo. Na kuepusha shari na balaa ya kidunia na kiakhera kwa kufuta maovu. "Na Mwenyezi Mungu ana habari ya mnayoyatenda." Kwa hivyo atamlipa kila mmoja kulingana na hekima yake.