Al-Baqara
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِٱلْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ 252
{252} "Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume." Na miongoni mwa ushahidi wa ujumbe wake ni kisa hiki, ambapo alikisimulia kwa ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kikilingana na namna kilivyotokea. Na katika kisa hiki kuna masomo mengi kwa umma huu: Miongoni mwake ni fadhila za jihadi katika njia yake, manufaa yake na matunda yake. Na kwamba ndio sababu pekee ya kuihifadhi dini, kuihifadhi nchi, kuihifadhi miili na mali. Na kwamba wanaopigana jihadi hata kama mambo ni magumu kwao, mwisho wao ni wa kusifika. Kama vile wale wanaofanya woga hata wakipumzika kidogo, wao kwa hakika watachoka kwa muda mrefu. Na miongoni mwake ni kukasimisha uongozi kwa yule ambaye ana uwezo, na kwamba uwezo huo unarudi kwa mambo mawili: Kwa elimu ambayo ni elimu ya kuongoza na kuendesha mambo, na kwa nguvu ambayo anatekeleza kwayo haki. Na kwamba yeyote ambaye mawili haya yamekutana ndani yake, basi yeye ndiye anayestahiki zaidi kuliko mwingine. Na miongoni mwake ni kukitumia kisa hiki kama dalili juu ya yale waliyoyasema wanachuoni. Kwamba amiri jeshi anatakiwa kuwakagua majeshi wakati wa kutoka. Ili amzuie asiyefaa kupigana vita miongoni mwa wanajeshi wanaopigana kwa miguu, na wapanda farasi, na wapanda magari kwa sababu ya udhaifu wake, au udhaifu wa subira yake. Au kwa sababu ya udanganyifu wake, au hofu ya kupata madhara katika kuandamana naye. Kwa sababu, kundi hilo ni madhara matupu kwa watu. Na miongoni mwake ni kwamba vita vinapokuwepo, inafaa kuwatia nguvu wanaopigana jihadi, na kuwatia moyo. Na kuwahimiza kuwa na nguvu ya kiimani na kumwachia kabisa Mwenyezi Mungu mambo na kumtegemea Yeye. Na kumwomba Mwenyezi Mungu uimara na msaada katika subira na ushindi juu ya maadui. Na miongoni mwake ni kwamba kuazimia kupigana vita na kufanya jihadi siyo (vita wala jihadi) yenyewe. Kwa sababu, mtu anaweza kuazimia, lakini anapohudhuria, azimio lake hilo linakatika. Na ndiyo maana katika dua za Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ni: "Ninakuomba uimara katika jambo hili, na azimio juu ya uwongofu.” Ndiyo hawa walioazimia kupigana vita, na wakaja na maneno yanayoonyesha azimio kubwa. Na muda ulipofika, wengi wao walighairi. Na hili linafanana na kauli yake (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. “Na ninakuomba ridhaa baada ya kunikatia jambo." Kwa sababu, kuridhika baada ya kupitishwa kwa jambo linalochukiwa na nafsi ndiyo ridhaa ya kweli.