Al-Baqara
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَآ أَنزَلْنَا مِنَ ٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلْهُدَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا بَيَّنَّـٰهُ لِلنَّاسِ فِى ٱلْكِتَـٰبِ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ يَلْعَنُهُمُ ٱللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ ٱللَّـٰعِنُونَ 159
Aya hii ijapokuwa iliteremshwa kuhusiana na watu wa Kitabu, na walichoficha katika hali ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na sifa zake. Ila hukumu yake ni ya jumla kwa kila mwenye sifa ya kuficha yale Mwenyezi Mungu aliteremsha, “katika hoja yaliyo wazi” zenye kuelekeza kwenye haki. Zenye kuidhihirisha, “na uwongofu” nayo ni elimu ambayo kwayo kunapatikana kuongoka kwenye njia iliyonyooka, na inabainisha kwayo njia ya watu wa neema kutokana na njia ya watu wa Motoni. Kwani, Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kutoka kwa watu wa elimu kwamba wawaelezee watu kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa katika elimu ya Kitabu, na wala wasiifiche. Kwa hivyo, mwenye kulitupa hilo, na akajumuisha kati ya maovu mawili, yani kuficha aliyoteremsha Mwenyezi Mungu na kuwapunja waja wa Mwenyezi Mungu, basi hao, “Mwenyezi Mungu anawalaani.” Yani anawaweka mbali na anawafukuza kutokuwa karibu naye, na rehema zake. “Na wanawalaani kila wenye kulaani.” Nao ni viumbe wote. Basi laana inawafikia kutoka kwa viumbe vyote, kwa sababu ya kufanya kwao juhudi katika kuwapunja viumbe na kuharibu dini zao, na kuwaweka mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, wakalipwa aina sawa na matendo yao. Sawa na vile mwenye kuwafundisha watu heri, anaswaliwa na Mwenyezi Mungu, na malaika wake, hata nyangumi ndani ya maji. Kwa sababu ya kufanya kwake juhudi katika masilahi ya viumbe, na kurekebisha dini zao, na kuwaleta karibu na rehema za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, akalipwa aina sawa na matendo yake. Kwa maana, mwenye kuficha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha anakwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, na anampinga Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anawabainishia watu Aya na anaziweka wazi, ilhali huyu anazifutilia mbali. Ndiyo maana, kuna tishio hili kali juu yake.