Al-Baqara
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوْ تَأْتِينَآ ءَايَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَـٰبَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ 118
(118) Yani: Walisema wajinga miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi kama alivyowasemesha Mitume "au zikatufikia Ishara." Wanamaanisha Aya za mapendekezo ambayo wanapendekeza kwa akili zao mbovu na rai zao potovu, ambazo walifanya ujasiri kwazo dhidi ya Muumba na wakawafanyia kiburi Mitume wake. Kama kauli yao, "hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi" (na) "Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo" hadi mwisho wa Aya. "Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye? Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale kutoka humo?" Hadi mwisho wa Aya hizi. Na kauli yake. "Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemichemi katika ardhi hii." Hadi mwisho wa Aya hizi. Basi haya ndiyo mazoea yao kwa Mitume wao, kutaka dalili za uasi, na sio dalili za uwongofu; na hayakuwa makusudio yao kubainishiwa haki. Kwani Mitume walikuja na Ishara ambazo mfano wake watu waliziamini. Na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Hakika sisi, tumeshazibainisha Ishara kwa watu wenye yakini." Hivyo basi, kila mwenye yakini alikwishajua kutokana na aya (ishara) za Mwenyezi Mungu zinazong'aa na dalili zilizo dhahiri, kilichomfanya kuwa na yakini; na inamwondokea kila shaka na kusitasita.