İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Maryam
Sure 19

Maryam

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

34–35. âyetler

ذَٰلِكَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ ٱلْحَقِّ ٱلَّذِى فِيهِ يَمْتَرُونَ 34 مَا كَانَ لِلَّهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ ۖ سُبْحَـٰنَهُۥٓ ۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ 35

{34-35} Yaani, huyo ni yule aliyesifiwa kwa sifa hizo, Isa mwana wa Maryamu, bila ya shaka wala kusitasita kokote, bali "ndiyo kauli ya haki" na neno la Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna neno ambalo ni la ukweli zaidi yake wala mazungumzo mazuri zaidi yake. Kwa hivyo, hii ndiyo habari ya yakini kuhusu Isa, amani iwe juu yake, na yote yaliyosemwa juu yake ambayo yanapingana na haya, hayo kwa hakika ni batili, na kiwango chake cha mwisho zaidi ni kwamba aliyeyasema ana shaka nayo na wala hana elimu yoyote kuhusiana nayo. Na ndiyo maana akasema, "ambayo wanaifanyia shaka." Yaani, wanatia shaka na kusitasita, na wanabishana kwa kukisia tu. Na miongoni mwao kuna anayesema juu yake kuwa: Yeye ni Mungu, au mwana wa Mungu, au wa tatu katika watatu, lakini Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya uzushi wao huo na kusema kwao uwongo huko. Basi "Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kujifanyia mwana." Yaani, haifai wala haiendani naye. Kwa sababu hili ni katika mambo yasiyowezekana, kwa maana Yeye ndiye Mkwasi, Msifika, mmiliki wa wamilikiwa wote. Basi vipi anaweza kujichukulia mwana kutoka kwa wamilikiwa wake? "Ametakasika"; Yaani: Ametakasika kutokana na mtoto na upungufu, "anapohukumia jambo" miongoni mwa mambo madogo na makubwa, basi haliwezi kukataa wala kumuwia gumu. "Yeye huliambia tu: Kuwa, na linakuwa." Basi ikiwa majaliwa yake na mapenzi yake yatatekelezeka katika ulimwengu wa juu na wa chini, basi vipi anaweza kuwa na mwana? Na ikiwa anapotaka kitu, anakiambia tu: Kuwa, na linakuwa, basi inawezaje kufikiriwa kwamba hawezi kumuumba Isa bila baba?