Al-Israa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِى هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰٓ أَكْثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورًا 89 وَقَالُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ ٱلْأَرْضِ يَنۢبُوعًا 90 أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ ٱلْأَنْهَـٰرَ خِلَـٰلَهَا تَفْجِيرًا 91 أَوْ تُسْقِطَ ٱلسَّمَآءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِىَ بِٱللَّهِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ قَبِيلًا 92 أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِى ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَـٰبًا نَّقْرَؤُهُۥ ۗ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّى هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا 93
{89-93} Yeye Mtukufu anasema, "Na hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano." Yaani, tumeeleza ndani yake aina mbalimbali za mawaidha na mifano, na tumerudiarudia humo maana ambazo waja wanazihitaji ili wazikumbuke na kumcha Mungu, lakini hawakukumbuka isipokuwa wachache tu miongoni mwao, wale ambao walikwisha andikiwa na Mwenyezi Mungu kwamba watakuwa wenye furaha, na Mwenyezi Mungu akawasaidia kwa kuwawezesha kufikia hayo. Ama wengi wa watu, hao walikataa isipokuwa kukufuru neema hii ambayo ndiyo kubwa zaidi kuliko neema zote, na wakaanza kumfanyia ukaidi kwa kutaka ishara zisizokuwa ishara zake, ambazo wanazizua kwa nafsi zao dhalimu zisizojua kitu. Wakamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ambaye alikuja na Qur-ani hii yenye kila hoja na ishara, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii." Yaani, mito itiririkayo. "Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu," ikawa inakutosheleza kwenda na kurudi sokoni. "Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai." Yaani, kipande cha adhabu. "Au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso," ili wakushuhudilie hayo uliyokuja nayo. "Au uwe na nyumba iliyopambwa" kwa dhahabu na vitu vingine. "Au upae mbinguni" kwa mwili wako. "Na" pamoja na haya, "hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome." Na kwa kuwa haya ni ukaidi, na kutaka kumfanya Mwenyezi Mungu kana kwamba hana uwezo, na ni maneno ambayo husemwa na watu wajinga zaidi na madhalimu zaidi, ambayo yanajumuisha kukataa haki na kuwa na tabia mbaya mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwamba Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - ndiye anayeleta tu ishara. Mwenyezi Mungu akamwamrisha amtakase, akasema, "Sema: Ametakasika Mola wangu Mlezi," kutokana na hayo mnayoyasema na yuko juu sana. Na ametakasika kutokana kwamba hukumu zake na ishara zake zifuatane na matamanio yao mabovu na rai zao potovu. "Je, kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu na Mtume," ambaye hana chochote mkononi mwake katika jambo hili?