İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ibrahim
Sure 14

Ibrahim

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 37

رَّبَّنَآ إِنِّىٓ أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِى بِوَادٍ غَيْرِ ذِى زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ ٱلْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجْعَلْ أَفْـِٔدَةً مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهْوِىٓ إِلَيْهِمْ وَٱرْزُقْهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ 37

{37} "Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria zangu katika bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu." Na hilo ni kwa sababu alimletea Hajar mama yake Ismail na mwanawe, Ismail, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake huku ananyonya baso, kutoka Sham mpaka akamuweka huko Makka. Nayo wakati huo ilikuwa hapakuwa na mahali pa kuishi wala mwitaji, wala mwitikiaji. Alipomuweka hapo, akamuomba Mola wake Mlezi kwa dua hii, akasema, akiomba dua kwa unyenyekevu na kumtegemea Mola wake Mlezi, "Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria zangu;" yaani, si dhuria yangu yote. Kwa sababu Is-haq alikuwa amebaki huko Sham na wanawe wengine pia. Lakini Ismaili tu na dhuria yake ndio aliwapa maskani huko Makka. Na kauli yake: "katika bonde lisilokuwa na mimea" ni kwa sababu ardhi ya Makka si nzuri kwa kilimo. "ili wasimamishe Swala;" yaani, wafanyeni wenye kukupwekesha, wenye kusimamisha Swala. Kwa sababu kusimamisha swala ni miongoni mwa ibada mahususi na bora zaidi za kidini. Kwa hivyo, Mwenye kuisimamisha, anakuwa ameisimamisha dini yake. "Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao." Yaani, ziwapende na kupenda mahali ambapo wanaishi. Basi Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake, na akatoa katika kizazi cha Ismail Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - mpaka akawalingania kizazi chake kwenye dini ya Kiislamu na mila ya baba yao Ibrahim, nao wakamwitikia na wakawa wanasimamisha Swala. Na Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufanya hijja kwenye nyumba hii ambayo Ibrahimu aliwaweka kuishi baadhi ya dhuria yake, na akaweka ndani yake siri ya ajabu ambayo iliivutia mioyo. Basi mioyo inaupenda na wala haikatiki haja yake juu yake daima dawamu; bali kila mja anapouendea kwa wingi, inazidi shauku yake, na hamu yake na utashi mkubwa. Na hii ndiyo siri ya Mwenyezi Mungu kuifungamanisha na nafsi yake takatifu. "Na waruzuku katika matunda, ili wapate kushukuru." Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake, na ikawa yanaletwa hapo matunda ya kila kitu. Na utaiona Makka tukufu kila wakati hali ya kuwa matunda ni mengi humo, na riziki zinaijia kutoka pande zote.