Yusuf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِى ٱلْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَآءُ ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَن نَّشَآءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ 56 وَلَأَجْرُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَكَانُوا۟ يَتَّقُونَ 57
{56-57} Yeye Mtukufu alisema: "Basi hivyo ndivyo;” yaani, kwa sababu hizi na utangulizi huu uliotajwa, "tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka” katika maisha ya starehe, na neema kunjufu, na heshima pana. “Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye;” yaani, haya ni katika rehema ya Mwenyezi Mungu kwa Yusuf ambazo alimpa na akamuandikia. Na hilo halikufungamana tu na neema ya dunia hii. Kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri. Naye Yusuf, amani iwe juu yake, ni miongoni mwa wakuu wa watenda mazuri. Basi ana mazuri katika dunia na Akhera pia ana mazuri, na ndiyo maana akasema: "Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi” - kuliko malipo ya dunia “kwa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu.” Yaani, kwa yule aliyekusanya kati ya uchamungu na imani. Kwa hivyo, kwa uchamungu yanaachwa mambo yaliyoharamishwa miongoni mwa madhambi makubwa na madogo yake. Nayo imani kamili inapatikana kwa moyo kusadikisha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha kukiaminiwa, na kufuatwa na matendo ya nyoyo na matendo ya viungo: yale ya wajibu na yale yanayopendekezwa.