Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sura ya 9

At-Tawba

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 7

كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَـٰهَدتُّمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۖ فَمَا ٱسْتَقَـٰمُوا۟ لَكُمْ فَٱسْتَقِيمُوا۟ لَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ 7

{7} Huku ni kubainisha hekima inayomfanya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kuwa mbali na washirikina, kwa hivyo akasema: "Vipi washirikina watakuwa na agano kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake." Je, walitekeleza wajibu wa imani? Au walimwacha Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini wasiwaudhi? Je, hawakupigana na haki na wakainusuru batili? Je, hawakuwania katika ardhi wakifanya uharibifu? Basi wanastahiki Mwenyezi Mungu kuwa mbali nao, na wala wasikuwe na agano lolote kwake wala kwa Mtume wake. "Isipokuwa wale mliofanya agano nao" miongoni mwa washirikina "kwenye Msikiti Mtakatifu," basi hao wana katika agano hilo - hasa katika pahali hapa penye ubora - utakatifu ambao ulilazimu wauzingatie ndani yake. "Basi maadamu watawawia wanyoofu, basi nanyi pia wawieni wanyoofu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamungu."