Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sura ya 9

At-Tawba

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 52

قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَآ إِلَّآ إِحْدَى ٱلْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ ٱللَّهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِۦٓ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوٓا۟ إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ 52

{52} Yaani, waambie wanafiki wanaokutazamia matukio mabaya: Ni kwa kitu gani mnatutazamia? Nyinyi hakika hamtutazamii isipokuwa jambo ambalo lina faida yetu kubwa zaidi, nalo ni moja ya mambo mawili mazuri haya: ima kuwashinda maadui na kupata nusura dhidi yao na kupata malipo ya kiakhera na ya kidunia, au kufa kishahidi, ambako ni miongoni mwa daraja za juu zaidi za viumbe na hadhi ya juu kabisa kwa Mwenyezi Mungu. Na ama kuwatazamia kwetu, enyi kundi la wanafiki, basi sisi "tunawatazamia kuwa Mwenyezi Mungu atawasibu kwa adhabu kutoka kwake" bila ya sisi kuwa ndiyo sababu ya hilo. "Au kwa mikono yetu" kwa kutupa sisi mamlaka juu yenu, tukawaua "Basi tazamieni" heri kwetu "nasi hakika tunatazamia pamoja nanyi" maovu yenu.