Al-Mursalaat
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَـٰكُمْ وَٱلْأَوَّلِينَ 38 فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ 39 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ 40
{38 - 40} "Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia" ili tupambanue baina yenu na tuhukumu baina ya viumbe. "Ikiwa mnayo hila" mnayoweza kufanya ili mtoke katika ufalme wangu na mkaepuka adhabu yangu kwa hayo, "basi nifanyieni hila Mimi!" Yaani, hamna uwezo wala mamlaka. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye pande za mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka." Basi Siku hiyo hila za madhalimu zitabatilika na vitatoweka, na watasalimu amri kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu, na uwongo wao utawabainikia katika kukadhibisha kwao. "Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!"