Al-Mumtahana
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا۟ لَكُمْ أَعْدَآءً وَيَبْسُطُوٓا۟ إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّوا۟ لَوْ تَكْفُرُونَ 2
{2} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha ukubwa wa uadui wao ili hilo liwachochee Waumini nao pia wawafanyie uadui: “Wakikuwezeni” wanapopata fursa ya kuwadhuru “wanakuwa maadui zenu” wa dhahiri, “na wanakukunjulieni mikono yao” kwa kuwaua, kumpiga na mfano wa hayo, “na ndimi zao kwa uovu” wenye kuwafanya msikie vibaya kama vile matusi na mambo mengine, “na wanapenda muwe makafiri” kwani hili ndilo lengo lao la mwisho wanalolitaka kwenu.