Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهْدِى بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا۟ لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ 88 أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحُكْمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰٓؤُلَآءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا۟ بِهَا بِكَـٰفِرِينَ 89
{88 - 89} "Huo," uwongofu uliotajwa "ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu," ambaye hakuna uwongofu isipokuwa uwongofu wake. "Anaongoa kwao amtakaye katika waja wake." Basi tafuteni uwongofu kutoka Kwake; kwani ikiwa hatawaongoa, basi hakuna wa kuwaongoa isipokuwa Yeye. Na miongoni mwa wale aliotaka kuwaongoa, ni hawa waliotajwa. "Na lau wangelimshirikisha," kama ingechukuliwa hivyo na kukadiriwa hivyo, "basi yangeliwaharibikia yale waliyokuwa wakiyatenda." Kwani ushirikina unabatilisha matendo, na unasababisha kudumu katika Moto. Basi ikiwa hawa wa hali ya juu sana, walio bora zaidi lau kuwa wangelimshirikisha, na haiwezekani hilo kwao –matendo yao yangeliharibika, basi wengine wanastahili hilo zaidi.