Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَحَآجَّهُۥ قَوْمُهُۥ ۚ قَالَ أَتُحَـٰٓجُّوٓنِّى فِى ٱللَّهِ وَقَدْ هَدَىٰنِ ۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّى شَيْـًٔا ۗ وَسِعَ رَبِّى كُلَّ شَىْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ 80
{80} "Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwisha niongoa?” Kuna faida gani katika kuhojiana na yule ambaye haujambainikia uwongofu? Na ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, na akafikia katika daraja za juu zaidi za yakini. Basi yeye mwenyewe anawalingania tu watu kwenda katika yale aliyo juu yake. "Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye." Kwani hawatanidhuru, wala hawatanizuilia chochote katika manufaa, "Isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?" Mkajua kwamba, Yeye peke yake ndiye muabudiwa anayestahiki kuabudiwa.