Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 76

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ ٱلَّيْلُ رَءَا كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى ۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلْـَٔافِلِينَ 76

{76} "Na ulipomuingilia usiku;" yaani, giza lilipoingia, "akaiona nyota," labda ni ilikuwa ni katika nyota angavu. Kwa sababu kuitaja kwa njia maalumu kunaashiria kuwa ni bora kuliko nyinginezo. Na ndiyo maana - na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye zaidi – akasema aliyesema kwamba ni Zuhura "Huyu ndiye Mola Mlezi wangu;" yaani, kwa namna ya kujishusha kwa daraja la mpinzani. Yaani, huyu ndiye Mola wangu Mlezi; basi njooni tuangalie: Je, anastahiki Umola? Na je, utasimama ushahidi wowote wetu kwa hilo? Kwani haimfailii mwenye akili timamu kuyachukua matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake bila ya uthibitisho wala hoja. "Na ilipotua;" yaani, nyota hiyo ilipotoweka; "Akasema: Siwapendi wanaotua.” Yaani, mwenye kutoweka na kufichikana kwa yule anayemwabudu. Kwa maana, muabudiwa ni lazima ayasimamie masilahi ya mwenye kumuabudu na kumuendeshea mambo yake yote. Ama yule ambaye unapita muda mwingi hali ya kuwa hayupo, basi ni vipi atastahiki kuabudiwa? Na je, kumchukua yeye kuwa mungu si isipokuwa upumbavu wa upumbavu wote, na batili ya batili zote?