Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sura ya 4

An-Nisaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 92

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَـًٔا ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَـًٔا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَصَّدَّقُوا۟ ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍۭ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَـٰقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ ٱللَّهِ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا 92

{92} Mbinu hii ni mojawapo ya mbinu za kutowezekana. Yani haiwezekani, na ni muhali kwamba itokee kwa Muumini kumuua Muumini mwingine, yani makusudi. Na katika hili kuna kujulisha ukali wa kuharamisha hilo, na kwamba ni linapingana na imani kupingana kukubwa mno. Lakini hilo linatoka kwa kafiri au kutoka kwa yule anayepita mipaka, ambaye imani yake imepungua kukupunguka kukubwa, na anahofiwa lililo kubwa zaidi kuliko hilo. Kwa maana, imani sahihi humzuia Muumini asimuue ndugu yake ambaye Mwenyezi Mungu ameweka kati yake na ndugu yake huyo undugu wa kiimani. Ambao miongoni mwa matakwa yake ni kumpenda na kumfanya rafiki mwandani, na kumwondolea chochote kinachoweza kumfikia ndugu yake miongoni mwa madhara. Na ni madhara gani makubwa zaidi kuliko kuua? Na hilo linasadikishwa na kauli yake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - “Msirudi baada yangu mkawa makafiri, mkapigana shingo nyinyi kwa nyinyi.” Basi, ikajulikana kuwa kuua ni katika ukafiri wa kimatendo, na dhambi kubwa zaidi miongoni mwa madhambi makubwa baada ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na wengine. Na ilipokuwa kauli yake, “Na haiwi Muumini kumuua Muumini” ni kauli ya jumla kwa hali zote, na kwamba halitoki kwake jambo la kumuua ndugu yake kwa namna yoyote ile, akatoa Yeye Mtukufu katika hilo kuua kimakosa. Akasema, “isipokuwa kwa kukosea;” kwani, mwenye kukosea ambaye hakukusudia kuua, si mtenda dhambi wala hakujasiri kufanya maharamisho ya Mwenyezi Mungu. Lakini kwa kuwa amefanya kitendo kiovu, na sura yake inatosha katika ubaya wake, hata kama hakukikusudia, Yeye Mtukufu akaamrisha kafara na diya (mali ya damu). Akasema, “Na mwenye kumuua Muumini kwa kukosea” sawa awe muuaji ni wa kiume au wa kike, huru au mtumwa, mdogo au mkubwa, mwenye akili timamu au mwendawazimu, Mwislamu au kafiri, inavyofahamika katika neno "mwenye," lenye kuonyesha ujumla. Na hili ni katika siri za kutumia "mwenye" katika pahali hapa. Kwani, muktadha wa maneno haya unamtaka aseme: Na iwapo atamuua,' lakini hili ni neno ambalo halijumuishi kile ambacho “mwenye” linajumuisha, na sawa aliyeuawa awe wa kiume au wa kike, au mdogo, au mkubwa, kama inavyofahamika kutokana na kutumia neno la kawaida katika muktadha wa sharti. Basi ni juu ya muuaji “amkomboe mtumwa aliye Muumini” kama kafara kwa ajili ya hilo, ambayo inatolewa kutoka katika mali yake. Na hilo linajumuisha mtoto na mtu mzima, wa kiume na wa kike, mwenye afya njema na mwenye kasoro, kulingana na kauli ya baadhi ya wanachuoni. Lakini hekima inahitaji kwamba isitosheleze kumuachilia huru mtu mwenye kasoro katika kafara. Kwa sababu kinacholengwa katika ukombozi ni kumfaidi yule aliyekombolewa na kummilikisha masilahi ya nafsi yake. Na ikiwa yanapotea kwa ukombozi wake, na kubaki kwake katika utumwa kuna manufaa zaidi kwake, basi haitoshelezi kumkomboa, ijapokuwa katika kauli yake, “amkomboe mtumwa” kuna kinachoonyesha hilo. Kwa sababu, ukombozi ni ukombozi wa yule ambaye manufaa yake yanastahili kupewa wengine ili yawe yake. Basi ikiwa hakuna faida ndani yake, haionekani kuwepo uwezekano wa ukombozi. Basi tafakari hilo, kwani liko wazi. Na ama kuhusu diya (pesa za damu), hiyo ni wajibu juu ya jamaa za muuaji katika kuuwa kwa kukosea na katika kuuwa kunakofanana na kwa makusudi. “Kuwapa jamaa zake maiti” ili kuzifariji nyoyo zao. Na maana ya “jamaa zake” hapa ni warithi wake. Kwa maana, warithi ndio wanaorithi yale aliyoyaacha miti. Kwa hivyo diya inaingia katika yale aliyoyaacha. Na diya ina maelezo mengi yaliyotajwa katika vitabu vya Fiqh. Na kauli yake, “isipokuwa waiache wenyewe kuwa ni sadaka,” yani warithi wa yule aliyeuawa waitoe kama sadaka kwa kusamehe kuchukua diya, kwa hivyo inaanguka. Na katika hilo kuna kuwahimiza kusamehe. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameiita sadaka, na sadaka inahitajika katika kila wakati. “Na akiwa” yule aliyeuawa “ni wa kutoka kwa kaumu ambao ni maadui zenu,” yani kutoka kwa makafiri wanaopigana vita na Waislamu “basi ni kwa kumkomboa mtumwa aliye Muumini,” na siyo lazima juu yenu kuwalipa diya jamaa zake. Kwa sababu ya kutoharamishwa kwao katika damu zao na mali zao. “Na akiwa” yule aliyeuawa “ni miongoni wa kaumu ambao kuna agano baina yenu na wao, basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini” na hilo ni kwa sababu ya uharamu wa jamaa zake kutokana na kile walicho nacho cha ahadi na agano. “Na asiyepata” mtumwa wala thamani yake, kwamba alikuwa na ugumu katika hilo, na hana kile kinachosalia chochote cha kutosha kumkomboa mtumwa baada ya hela za matumizi yake na mahitaji yake ya asili; “basi afunge miezi miwili mfululizo.” Yani asifungue saumu baina yake bila ya udhuru, kwa sababu udhuru haukatizi mfululizo, kama vile maradhi, na hedhi, na mfano wake. Na kama kwa sababu isiyokuwa udhuru, basi mfululizo unakatika, na inamlazimu kuanza tena kufunga saumu. “Iwe ni kuitikiwa toba yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Yani hizi kafara ambazo Mwenyezi Mungu alizifaradhisha juu ya muuaji ni ili aitikiwe toba yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya waja wake na kwa ajili ya kuwarehemu, na kuwafutia dhambi kwa sababu ya kile kinachoweza kutoka kwa cha kupuuza, na kutotahadhari, kama ulivyo ukweli mara nyingi kwa mwenye kuua kwa kukosea. “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima kubwa.” Yani mwenye elimu kamili, mwenye hekima kamili, haufichiki kwake uzito wa chembe katika ardhi wala katika mbingu, wala kilicho kidogo zaidi kuliko hicho, wala kikubwa zaidi katika wakati wowote ule au mahali popote pale, wala hakuna kitu kilicho nje ya hekima yake miongoni mwa viumbe vyake na sheria. Bali kila alichokiumba na kukiweka kama sheria kinajumuisha hekima ya juu kabisa. Na katika elimu yake na hekima yake ni kwamba alimwajibishia muuaji kutoa kafara inayolingana na kile alichofanya. Kwani, alisababisha kufa kwa nafsi iliyoharamishwa, na kumtoa kwenye kuwepo hadi kwenye kutokuwepo. Basi ikafaa kwamba amwachilie huru mtumwa na kumtoa katika utumwa kwa viumbe hadi katika uhuru kamili. Na asipopata huyu mtumwa, atafunga miezi miwili mfululizo. Kwa hivyo akajiondoa katika utumwa wa matamanio na ladha za kihisia ambazo zilimkatia mja furaha yake ya milele, hadi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuziacha ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliliwekea muda huu mrefu, mgumu katika idadi yake na uwajibu wa kuzifululiza, na hakuweka sheria ya kulisha katika hali hizi kwa sababu kulifaiana nazo. Tofauti na Dhihar, kama itakavyokuja, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda. Na hakika hekima yake ni kwamba alilazimisha diya katika kuua, hata ikiwa ni kwa kukosea, ili hilo liwe kemeo na kizuizi kutokana na mauaji mengi kwa kutumia sababu za kuzuia kufanya hivyo. Na miongoni mwa hekima zake ni kuwa diya ililazimishwa juu ya jamaa za muuaji kuua kwa kukosea, kulingana na makubaliano ya wanachuoni. Kwa sababu muuaji hakutenda dhambi, na ingekuwa vigumu kwake kubeba diya hii nzito, kwa hivyo ikafaa kwamba wafanye hivyo wale ambao kati yake na wao kuna kufanya kwa pamoja, na kunusuriana, na kusaidiana katika kufikia masilahi na kuzuia maovu. Na huenda hilo ni mojawapo ya sababu za wao kumzuia yule ambaye wanamsaidia kulipa diya kutokana na kuua ili kujihadharisha kuwabebesha hilo, na linakuwa jepesi kwao kwa sababau wanagawiana kati yao kulingana na hali zao na uwezo wao, na pia kwa sababu ya kuiahirisha kwa miaka mitatu. Na katika hekima yake na elimu yake ni kwamba aliwafariji jamaa za yule aliyeuawa kwa msiba wao kwa diya ambayo aliiwajibisha kwa walinzi wa muuaji.