An-Nisaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِۦ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفْتَرَىٰٓ إِثْمًا عَظِيمًا 48
{48} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye hamfutii dhambi mwenye kumshirikisha na chochote katika viumbe, na hufuta yale yaliyo chini ya hilo miongoni mwa madhambi; madogo yake na makubwa yake, na hilo ni anapotaka kuyafuta hayo ikiwa hekima yake inataka kuyafuta. Kwa hivyo, dhambi ambazo ni ndogo kuliko ushirikina, Mwenyezi Mungu aliziwekea sababu nyingi za kufutwa kwake, kama vile matendo mema yanayoyafuta, na misiba yenye kusitiri dhambi katika dunia hii, na kaburini, na Siku ya Qiyama. Na kama vile dua ya Waumini wao kwa wao, na uombezi wa waombezi, na juu ya hayo yote ni rehema yake ambayo wanaoistahiki zaidi ni watu wa imani na Tauhidi. Na hii ni tofauti na ushirikina; kwa maana, mshirikina amejifungia milango ya kufutiwa dhambi, na akajifungia nje ya milango ya rehema. Basi utiifu haumnufaishi pasi na Tauhidi, wala misiba haimnufaishi kitu. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, "Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika amezua dhambi kubwa," yani amezua kosa kubwa. Na ni dhuluma gani kubwa kuliko yule aliyemsawazisha kiumbe aliyeumbwa kutoka katika udongo, aliye mpungufu katika namna zote, fakiri yeye mwenyewe kwa namna zote, ambaye haimilikii nafsi yake mbali na yule ambaye yeye anamuabudu faida yoyote wala madhara, wala kifo, wala uzima, wala ufufuo na yule ambaye mkononi mwake ndimo kuna manufaa na madhara, na kutoa na kuzuia? Na ambaye hakuna neema yoyote waliyo nayo viumbe isipokuwa ni kutoka kwake Yeye Mtukufu? Basi je, kuna kitu kikubwa zaidi kuliko dhuluma hii? Na kwa sababu hii, ndiyo akapitisha kwa mwenye haya kudumu katika adhabu, na kunyimwa thawabu, "Hakika, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu ameshamharimishia Pepo, na kimbilio lake ni Motoni." Na Aya hii tukufu inahusiana na yule ambaye hakutubia. Na ama aliyetubia, basi yeye anafutiwa dhambi ya shirki na yaliyo chini yake, kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Sema: Enyi waja wangu waliopitiliza mipaka dhidi ya nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu hufuta dhambi zote."