Az-Zumar
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
قُلْ يَـٰقَوْمِ ٱعْمَلُوا۟ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّى عَـٰمِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ 39 مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ 40
{39 - 40} Yaani, "Sema" ukiwaambia ewe Mtume: "Enyi watu wangu! Fanyeni muwezavyo" kwa kusalia katika hali zenu mlizoziridhia nafsi zenu za kumuabudu, asiyestahiki ibada yoyote wala hana mamlaka yoyote katika hilo. "Mimi pia nafanya" kwa mujibu wa yale niliyokuitieni ya kukusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika dini. "Basi mtakuja ona" ni nani atakayekuwa na mwisho mwema, "na ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi" katika dunia hii "na itakayemshukia adhabu ya daima" ambayo haitawahi kuondoka wala kwisha. Hili ni tishio kubwa kwao, kwani wanajua vyema kwamba wao ndio wanaostahiki adhabu ya milele, lakini dhuluma na ukaidi vikawazuia kuamini.