Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ya 39

Az-Zumar

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 22

أَفَمَن شَرَحَ ٱللَّهُ صَدْرَهُۥ لِلْإِسْلَـٰمِ فَهُوَ عَلَىٰ نُورٍ مِّن رَّبِّهِۦ ۚ فَوَيْلٌ لِّلْقَـٰسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ ٱللَّهِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ 22

{22} Yaani, je, ni sawa yule ambaye Mwenyezi Mungu amekifungua kifua chake kwa Uislamu, kwa hivyo kikapanuka ili kupokea hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzifanyia kazi kwa uwazi, furaha, na ufahamu mzuri wa mambo yake, naye ndiye aliyekusudiwa na kauli yake, "na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi," ni sawa na asiyekuwa hivyo, ambaye moyo wake ni mgumu? Kama ilivyosema: "Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu!" Hazilainiki kwa ajili ya Kitabu chake, wala hazikumbuki aya zake, na wala hazipati utulivu katika kumkumbuka, bali zinajiepusha na Mola wake Mlezi na kuwaelekea wengineo. Hawa wanapatwa na balaa na uovu mkubwa. Na "hao wamo katika upotofu wa dhahiri." Na ni upotofu gani ulio mkubwa zaidi kuliko upotevu wa mwenye kumpa mgongo mlinzi wake, na yule ambaye furaha yote iko katika kurejea kwake, na moyo wake ukawa mgumu usimtaje, na akayaendea kila yenye kumdhuru?