Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ya 39

Az-Zumar

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 14–15

قُلِ ٱللَّهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُۥ دِينِى 14 فَٱعْبُدُوا۟ مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِۦ ۗ قُلْ إِنَّ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْخُسْرَانُ ٱلْمُبِينُ 15

{14 - 15} "Sema: 'Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu. Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye." Kama alivyosema: "Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnachokiabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu." "Sema: Hakika waliohasirika" kwa uhakika ni "wale waliojihasiri nafsi zao" kwa kuwa walizinyima thawabu na zikastahiki kwa sababu yao adhabu kali, "na ahali zao Siku ya Kiyama." Yaani, watatenganishwa na huzuni yao na hasara yao itakuwa kubwa. "Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri," ambayo hakuna hasara nyingine mfano wake. Ni hasara inayoendelea ambayo hakuna faida yoyote baada yake, wala hata hakuna usalama.